Machi 31, 2021
Dakika 3. Soma

Fumba Mbili-Wazo Moja

Tafuta maeneo yote mapya yenye maendeleo yanayovutia kando ya bahari nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Yote haya yanatokea katika peninsula ya Fumba: Maendeleo ya maeneo mawili makubwa ya uendelezaji miji yameanzisha fursa za maisha ya kisasa kwa majengo ya nyumba za kitalii na nyumba za kudumu za familia karibu na mji mkuu wenye msongamano wa watu.

Na ANDREA TAPPER

Maeneo yote mawili ya jumuia kando ya bahari, yalianzishwa mwaka 2015/16, na kuvutia wakazi wenyeji pamoja na idadi ya wageni wa kimataifa wanaoongezeka na wawekezaji. “Mpaka sasa tuna wanunuzi kutoka mataifa 57”, anasema Sebastian Dietzold, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa CPS, waendelezaji wa Fumba Town. “Tuna mengi ya pamoja kuliko yanayotutenganisha”, anasisitiza Saeed A. Bakhressa, mkurugenzi wa mradi wa Fumba Uptown Living (FUL) unaoendelezwa na kundi la makampuni ya Azam Bakhresa, kampuni kubwa maarufu ya Kiafrika. “Yote inahusu imani na dira ya kuifungua Zanzibar”, wawekezaji wote wawili wanakubali hilo.

Kwa hiyo, nini tofauti kati ya Fumba Town na majirani zetu Fumba Uptown - na nini kinawaunganisha wawekezaji hawa katika kisiwa hiki? Wapi mahali pazuri zaidi pa kufanya manunuzi ukiwa katika nyumba ya mapumziko au nyumba ya kudumu ya familia? Vema, inaanza na kionjo …na huenda inamalizikia na uwezo wako wa kifedha(see box). Wakati miradi yote miwili inalenga ‘’kukidhi mahitaji makubwa ya nyumba katika Zanzibar” (Dietzold), ahadi ”matokeo ya juu katika uwekezaji” (Bakhressa) na kusaidia viwanda vya ndani na ajira, mmoja anaweza - kwa lengo tu la kutofautisha – tambua aina ya mradi wa uptown kama kwa kiasi fulani mzuri zaidi na wa kawaida, na Fumba Town unajitambulisha kwa mwonekano wa kijani zaidi kutokana na bustani za miti na kitu cha majaribio zaidi. 

Ni miradi ya mazingira dhidi ya mradi wa kifahari, halafu? Hiyo itafanya kuwa rahisi. Fumba Town imeibuka kutoka ardhi kame ya mwamba wa matumbawe kugeuzwa katika eneo la kuvutia la mimea ya kitropiki katika muda wa miaka mitatu tu kwa matumizi bora ya ardhi yanayozingatia kilimo hai, Lakini ushindani wa uptown unaweza pia kujivunia kuwa na maji yake na mitambo ya umeme inayozalisha umeme wa kufikia megawatt 20 na kuzalisha maji ya kunywa yapatayo lita milioni tatu. “Kando ya hapo, miji yote miwili inakabiliwa na changamoto za aina moja”, anasema Bakhressa. Upungufu wa mchanga unachelewesha mchakato wa ujenzi. Changamoto nyingine: “Uturuki au Mauritius imeweka haraka ruzuku ya makazi kwa wanunuzi wa nyumb, katika Zanzibar bado tunasisitiza hilo kufanyika”, Bakhresa mwenye umri wa miaka 41 anabainisha. 

Ukitumia mfumo wa kuzunguka katika viunga vya kushangaza vya Uptown pembezoni mwa jbali, una burudika na upepo mwanana kutoka katika bahari. Kilomita chache, wateja utakuta wakifurahi wakiomba punguzo la bei katika mtaa maarufu wa soko katika Fumba Town, wakichagua kati ya jemu za matunda zilitengenezwa majumbani na mafuta ya ngozi ya Aloe Vera. Tayari kuna maisha ya yanayoonekana ya ukaazi wa watu katika Fumba Town, ambako majengo yapatayo 500 yenye jumla ya nyumba 3000 ambazo zimejengwa katika mitindo tofauti na bei tofauti tayari zimeuzwa na nyingine zimekaliwa – zikiwa katika bei ya chini kwa nyumba ndogo hadi nyumba kubwa za mjini kufikia ghorofa tatu. 

Kwa upande wake katika mradi wa Uptown Living, nyumba za kifahari zikiwa na umiliki wa mtu binafsi na jengo la ghorofa kumi ni kivutio kwa wanunuzi wa baadaye. “Tunauza nyumba ambazo tu ziko tayari kukabidhiwa”, anaelezea mkurugenzi Bakhressa, “ukamilishaji wa ujenzi bado unaendelea na bado hatujaanza kutangaza”. Fumba Town inauza nyumba kabla hazijajengwa; wanunuzi wanalipa kidogo kidogo.

Furaha ya mwanzo mpya inaonekana kwa miradi yote miwili. “Sikuweza kuamini macho yangu kuona miji hiyo miwili ikiibuka katika eneo lisilotarajiwa”, mgeni mmoja anasema. Na wawekezaji wote wawili wa miji hiyo wanaonekana kukubaliana: Kama kisiwa cha Manhattan jijini New York kuna eneo la juu, kati na eneo la chini, miji hiyo miwili ya kitropiki katika peninsula ya Fumba hatimaye huenda ikaunda kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Zanzibar- kikiwa na ujirani tofauti lakini kikiwa na ahadi inayokiunganisha ya maisha bora katika Zanzibar! 

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Julai 15, 2024
2 dakika.

CHAGUA SARADINI, EPUKA KASI

Mwongozo wa ulinzi wa AZ: ninaweza kula samaki gani? Baadhi ya vyakula vitamu zaidi Zanzibar ni pamoja na dagaa – si jambo la kushangaza kisiwani. Lakini aina fulani za samaki ziko chini ya tishio, hata hapa. Kisiwa cha Chumbe, mahali pa likizo ya kijani kibichi zaidi Zanzibar, kimekuja na mwongozo wa vitendo wa vyakula vya baharini vya kaya. Burger ya samaki na tangawizi na ufuta? Inayo ukoko wa joto […]
Soma zaidi
Julai 9, 2024
3 dakika.

AINA TOFAUTI YA SHULE

Mfululizo mpya: Kuishi na watoto Zanzibar Je, ni lazima mtu aje barani Afrika kutafuta shule ambazo hazijakamilika? Ilianzishwa na wazazi, shule ndogo ya pwani huko Jambiani inaweka viwango vipya. Saa nane na nusu, na shule huanza na mkusanyiko wa shule na kuimba kwa pamoja. Watoto wameingia kimya kimya, kila mmoja akinawa mikono […]
Soma zaidi
Julai 4, 2024
2 dakika.

HATIMAYE WAKAZI

Wamiliki wa nyumba wa kwanza kupata makazi Zanzibar. Furaha na ahueni zilionyeshwa wakati wamiliki wa kwanza wa nyumba za kigeni walipopewa hati ya ukaaji halali mwezi Mei mjini Zanzibar. Wote wanne ni raia wa Uholanzi na wamenunua eneo hilo katika Mji wa Fumba, mji unaokua wa mazingira karibu na mji mkuu. Hali mpya ya makazi inatolewa na uwekezaji […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

Maswali 25 muhimu na majibu ya kununua mali Zanzibar

SOMA ZAIDI
Whatsapp Nasi