Mei 18, 2021
Dakika 3. Soma

Inavutia sana

Sharmin Esmail ameleta haiba na mtindo kwa wadhifa wa juu wa meneja wa mji.

Kwa mara ya kwanza nafasi hiyo ya kipekee ya meneja wa mji katika Fumba Town imejazwa na mwanamke - akiongeza haiba hiyo nzuri, lakini tofauti muhimu ni uwepo wa mwanamke.

Sharmin Esmail akiingia katika nyumba yake maridhawa Fumba Town. Na kwa hiyo, tukiachana na msemo wa kawaida, anawahudumia wageni wanapofika katika ofisi yake. Meneja huyo wa mji mwenye umri wa miaka 48 ni mmoja wa watu wachache ambao uwepo wao unakufanya moja kwa moja ujisikie mtulivu, uko huru na zaidi ya yote, unahudumiwa kikamilifu. Anaonekana kuangazia sifa za ubora kwa nafasi yake ya kipekee ya kusimamia mji mzima! Sehemu mtawala, sehemu mmiliki wa nyumba, sehemu msimamizi wa nyumba, sehemu mwana mitindo na – mwisho lakini si kwa umuhimu – mtu mwenye akili ya mawasiliano akiwa na elimu nzuri ya ufundi na uendeshaji: Nafasi ya Sharmin inahusisha maelezo ya kazi zote hizi. Lakini wakati namwuliza binafsi anavyoweza kueleza mipango yake katika Fumba Town kwa maneno machache, anaeleza kama suala rahisi zaidi kuliko uhalisia ulivyo: “Nataka kila kitu kivutie”, anasema na kunipa tabasamu.

Msimamizi wa sehemu, mwenye nyumba, msimamizi wa sehemu, mtunzi wa sehemu na - mwisho kabisa - mwanamtandao mwerevu na ujuzi wa kutosha wa kiufundi na shirika: Nafasi ya Sharmin inajumuisha maelezo haya yote ya kazi. Lakini ninapomuuliza jinsi yeye binafsi angeelezea misheni yake katika Mji wa Fumba kwa maneno machache, anaiacha isikike rahisi zaidi kuliko ilivyo hakika: “Nataka tu kila kitu kiwe cha kukaribisha”, anasema na kunipa moyo- tabasamu la joto.

Katika ufuo wa kipekee wa mji wa Fumba, wenye ongezeko la watu na sekta kubwa ya maendeleo ya mazingira ukiwa bado katika mipango na ujenzi, mzigo wa kazi yake hauna kikomo: Akiwa na timu ya watu kumi, meneja huyu wa mji wa Fumba anaangalia namna ya kuimarisha miundombinu ya umma na matumizi ya mtandao wa internet wenye kasi ya juu na maji salama. Anakagua mandhari, anasimamia na kuandaa matukio kama vile gulio la wazi la kila mwezi na senema za usiku. Pia, mhitimu huyo wa maendeleo ya raslimali watu na saikolojia ya watoto anahakikisha usalama wa watoto unaangaliwa wakati wote na ndiye aliyeweka alama za barabarani katika eneo hilo jipya la makazi na biashara. Nyingine ya kazi zake ni kupanga ukodishaji wa nyumba na majengo kwa niaba ya wamiliki wake. Kuelekea mwisho, Esmail ameanzisha kampuni ndogo ya mitindo na mapambo ikiitwa “Iman” kwa majengo ya mtindo binafsi na nyumba na ukamilishaji wa nyumba. Hii imethibitisha mafanikio ya moja kwa moja na wenye nyumba ambao hawaishi Zanzibar na kuhitaji mtaalamu mmoja wa kutunza nyumba zao.

“Napenda rangi ya kijani na bluu, rangi za bahari”, anasema Sharmin, wakati akinionyesha nyumba yake ya vyumba viwili vya kulala ambavyo vimepambwa kwa unadhifu iliyoko Fumba. Alihamia hapa alipo alipopata kazi chini ya mwaka mmoja uliopita, nyumba nzima imechangamka na usimamizi wa mwanamke. Ni mama wa watoto wawili na mfanyakazi wakati huo huo, Sharmin anaelewa thamani ya kampuni makini. “Ikiwa nadhifu, hakuna kazi kubwa”, anasema. Anaishi Washington DC, New York na Florida kwa miaka tisa ambako nako anajishughulisha na biashara ya nyumba na majengo. Jijini Dar es Salaam, alikozaliwa na kukulia, anajulikana vizuri kwa kazi yake ya huduma ya usafi “Spiknspan”. “Nilipoanza kazi hiyo kila mtu alinicheka”, anakumbuka – kwa sasa huduma hii iliyostawi imeajiri wahudumu wa usafi 800 ambao wanahudumia nyumba binafsi, mashirika ya ndege, na hata Ikulu na ina shughuli zake Marekani.

Akilinganisha maisha yake ya shughuli nyingi huko Marekani na yale ya utulivu katika Fumba, Esmail anasema: “Siikumbuki kabisa Marekani. Nikiwa Washington, nilikuwa nahangaika kuendesha gari kwenda kwenye viunga vya mapumziko,hapa naishi katika mojawapo ya viunga!” Kushuhudia furaha na vifijo vya wamiliki wa nyumba wakati wa kukabidhi nyumba mpya ni moja ya wajibu wake – “ni zawadi kubwa”, anasema, akiongeza: “Nafurahia sana kazi yangu, haionekani kama moja.” Paka wanaonekana kukubaliana na hili, wakijinyosha nyosha wakati wakionekana kusikiliza mazungumzo yetu.

Rangi za bahari: nyumba nadhifu iliyobuniwa na kampuni ya Iman ya Sharmin.

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Fumba Mbili-Wazo Moja

Find out all about new exciting seaside developments just outside Zanzibar city It’s all happening on the Fumba peninsula: Two major real estate developments creating modern living space with holiday flats and permanent family homes near the overcrowded capital. By ANDREA TAPPER Both aspiring seaside communities, started in 2015/16, fascinate locals as well as a […]
Soma zaidi
Aprili 15, 2024
3 dakika.

"ZANZIBAR IS SO SUBLIME"

The son of Femi Kuti and grandson of Fela Kuti headlined one of the best Busara festivals ever By Andrea Tapper  He flew into Zanzibar, capturing the hearts of music fans from all over. Afrobeat musician Mádé Kuti, 28, and his wife Inedoye, 25, made time for an exclusive interview with THE FUMBA TIMES before […]
Soma zaidi
Aprili 12, 2024
2 dakika.

MANHATTAN MEETS FUMBA

Manhattan is 14.6 kilometres long and 3.5 km wide. Fumba is 14.3 kilometres long and 3.6 km wide. Otherwise, the two peninsulas couldn’t be more different, of course. Glitzy Manhattan, one of the commercial and cultural centres of the world, full of skyscrapers, banks, offices, residential skyscrapers. Fumba in Zanzibar, still green and rural, showing […]
Soma zaidi
Aprili 8, 2024
4 dakika.

HAS THE WEATHER GONE CRAZY?

EXCLUSIVE INTERVIEW Incredible heat, endless rains – has the weather gone crazy? THE FUMBA TIMES editor-in-chief Andrea Tapper asked a man who knows a lot about the climate in Zanzibar: Hassan Khatib Ame, 44, head meteorologist at the international airport. THE FUMBA TIMES: Am I wrong, or has it been even hotter and more humid […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

25 essential questions and answers to buy property in Zanzibar

READ MORE
Whatsapp Nasi