Oktoba 13, 2021
Dakika 5. Soma

Milango, Birika za Chai na Blauzi za Lesi

Katika duka la manunuzi katika maeneo manne(4)

Mahali pasipo na maduka ya Gucci wala Zara, bidhaa za mitumba kwa matumizi ya nyumbani na urembo ni bidhaa mbadala za kuvutia. Gundua mauzo ya vito nje ya Stone Town ukiongozwa na Said. 

Birika za chai zikiwa na rangi ya michoro ya maua na matumbawe, zikiwa na mhuri wa China katika kitako chake zinapendeza lakini hazina mfuniko. “Inawezekana zinatoka miaka ya hamsini”, anasema Bernadette Kirsch. Mwavuli unaopitisha mwanga una mshinikio usio imara, ambao ni dhahiri hauwezi kuhimili upepo mkali wa kuzi au kaskazi “Usijali”, muuza duka mwenzangu amenishauri, “unaweza kutumia birika ya chai kumwagilia maua badala ya chupa ya plastiki ya kumwagilia maji, na unaweza kustawisha miche yako chini ya mwavuli”. Tupo watatu, Bernadette, mwongozaji wetu Said Suleiman na mimi mwenyewe - tukitafuta baadhi ya vitu vizuri vya kale!

Maumbo yanafuatana na kazi(mbunifu anasema), na wanawake wanapenda maumbo mazuri ya vitu. Wako tayari kutoa vitu vya thamani kama maisha mapya, mara kwa mara wakivibadili matumizi yake pia. Mkurugenzi wa kliniki ya Fumba Dkt. Jenny Bouraima aliwahi kugundua sofa iliyochakaa pembezoni mwa barabara mjini Zanzibar, Aliomba kuuziwa na kuibadili kwa kitambaa chenye mwonekano wa ngozi inayonga’aa. Sofa hiyo sasa inatumika kukaliwa na wagonjwa wake katika eneo la mapokezi. 

Sahani za udongo kutoka Uholanzi, birika za chai kutoka China na blauzi zenye lesi kutoka zama zilizopita za simulizi za historia ya Zanzibar, ya karne nyingi zilizopita za biashara ya Sofara wakati wa pepo za monsuni na nchi za Kiajemi, India, Arabuni na Uingereza. Samani za kale za utamaduni wa Waswahili zilipata nafasi ya kuupambanua utamaduni wake katika Afrika Mashariki. Baadhi zikiwa ni samani zilizotumika, hata hivyo, zungumzia habari za sera za sasa za utupaji vitu. Uingizaji wa bidhaa za mitumba kutoka nchi zilizoendelea na zinazoendelea umekosolewa kwa kiasi kikubwa. “Watu wanasema bidhaa za mitumba zinaharibu sekta ya viwanda vya ndani”, anafahamu Bernadette Kirsch, mkuu wa kampuni ya Ubunifu wa Kilimo Endelevu(PCD) iliyoko Fumba na kutoa mwangwi wa aina yake kuhusu bidhaa hizo katika jamii. “Lakini kwa kuwa hakuna mbadala halisi, yaani viwanda vyenye kutengeneza bidhaa za kiwango hicho cha ubora, biashara ya mitumba inazalisha kipato kwa watu wengi”, anasema.

Kwa hiyo, ziara yetu katika vitongoji vya Mji Mkongwe(Stone Town) iko tayari kuanza! 

KITUO CHA KWANZA (FIRST STOP) Kituo chetu cha kwanza ni katika ghala wazi ambalo pia ni karakana katika eneo la Fuoni ambako mfanyabiashara maarufu wa bidhaa za kale kutoka Stone Town anaweka na kuhifadhi bidhaa anazopata. Tukiwa njiani kuelekea Tamin, katika barabara ya Mombasa, wakati wote mwongozaji wetu Said alikuwa akionyesha majina ya maeneo tofauti tofauti jirani yanayotambulisha watu waliomkaribisha, “Mchina”, jengo jipya limepewa jina bandia la Mchina; maeneo mengine yanaitwa Mombasa, Somalia, hata “Kosovo”. 

Katika ghala la Tamin utakuta milango iliyochongwa kwa ustadi wa hali ya juu ipatayo kumi mbili, bawaba za madirisha zilizoingia kutu, fremu za mbao zenye mwonekano chakavu na uzio wa chuma ulioingia kutu vimetapakaa kila mahali. “Milango iliyochongwa yenye utambulisho wa Zanzibar, mingi ikiwa na umri wa miaka mia moja hadi 120, lakini mingine miaka 300 nyuma, inalindwa na sheria za urithi wa mambo ya kale”, anaelezea Said wakati anatuona tunashangaa hazina hiyo. “Ni marufuku kuisafirisha nje, lakini mtu anaweza kupata kwa matumizi ya ndani”. Wakati wa miaka 200 ya utawala wa Sultan, wakati makazi yake yalijengwa Zanzibar, mlango ulichongwa kwanza kijadi, anaeleza Said: “Mlango ulikuwa zaidi ya mlango, ulikuwa utambulisho wa kibiashara wa mmiliki”. Milango ya jadi 200-500 idadi inabadilika kutokana na makadirio tofauti - bado inatumika katika Mji Mkongwe (Stone Town). Fremu ya juu ya mviringo ilikuwa inaelekezwa kwa mmiliki wa Kihindi, fremu ya mraba kwa mmiliki wa Omani na mchanganyiko wa maumbo hayo ulikuwa kwa Waswahili. Uchongaji huu mara nyingi uliashiria taaluma ya mmiliki, mathalan kamba za kufungia meli, nahodha wa meli aliyesimama, zabibu au nyayo za mnyama zikionyesha maisha kabla ya ujio wa dini ya Kiislamu kwa sababu mvinyo na sanamu za wanyama ni haramu katika imani ya Kiislamu. Mlango wa kale kwa sasa unauzwa dola za Kimarekani $1000 katika soko

Baadhi ya maduka ya vitu vilivyotumika na mauzo madogo tuligundua kuwa hata majina havina. Maduka mengi ni ya vitu vya vibanda vya mtaani, mengine ni ya mauzo ya vitu vyao, kutoka vifaa vya vipandikizi hadi vyombo, kutoka mikoba ya wanawake hadi midori ya watoto, vikiwa vimewekwa kwenye blanketi la zamani au karatasi ya plastiki ikiwa imetandikwa chini. Bernadette na mimi tumefarijika sana kuwa na Said Suleiman kama mwongozaji wetu ambaye anaufahamu mji barabara, la sivyo tusingeweza kugundua maduka haya. Said anaweza kuombwa kuwa mwongozaji wa safari za kitalii za aina hii, kutoka utalii wa mashamba ya mazao ya viungo hadi maduka madogo kama yetu(angalia kisanduku kwenye ukurasa huu). 

Ametuleta kwenye baadhi ya nguzo za biashara za maduka ya vitu vilivyotumika

- katika barabara ya Mombasa kutoka mzunguko wa barabara wa Fumba kwenda Mwanakeregwe, tukiwa na vifaa vilivyotumika vya ujenzi, mimea na samani ndogo

- barabara nzima ya Fumba, baiskeli za watoto, samani, nguo za jumla

- katika barabara ya kwenda uwanja wa ndege, kukiwa na bidhaa za viti na meza, midori ya watoto, nguo za mitumba.

KITUO CHA PILI.(SECOND STOP) Wakati huo huo katika eneo la Mpendae, tuliona bidhaa zilizosambazwa chini na muuzaji. Mbele ya kibanda cha mbao anauza bidhaa mbalimbali zikiwemo za bilauri, visahani vya kuwekea majivu ya sigara, sahani za chakula zikiwa na mwelekeo wa Kijerumani, mikoba ya kusafiria na bakuri ndogo za Kichina zikiwa zimeandikwa “Royal Stafford, made in England 1845”. Kwa kweli siwezi kujizuia kununua bidhaa za Royal Stafford na zinauzwa kwa shilingi 3000 tu za Kitanzania (TZS 3000). Kweli tulinunua!

KITUO CHA TATU.(THIRD STOP) Zaidi kuhusu mfumo tata wa biashara ya vitu vilivyotumika unamwibua kwetu Sultan Huney akifanya biashara ya jumla ya bidhaa za asili ya India katika barabara ya Fumba. Zikiwa mlima wa bidhaa zilizofungwa na zisizo fungwa, kutoka baiskeli za watoto hadi mikoba ya mkononi hadi vyombo vya udongo, anaeleza: “Tunapokea kasha la vipande 800 visivyojulikana ni nini kwa gharama ya shilingi za Kitanzania TZS 400,000, tunauza kwa gharama ya shilingi TZS 900,000. Muuzaji wa rejareja anachagua bidhaa zetu na kuziuza upya moja baada ya nyingine. Endapo mtu anataka vipande vilivyochambuliwa nasi kabla, bei inaongezeka.” Mfanyabiashara wa barabara ya Fumba ana duka lake la rejareja. Awali lilikuwa katika barabara ya Fumba, sasa limehamia eneo la Mazizini karibu na kituo cha polisi. 

KITUO CHA NNE.(FOURTH STOP) Blauzi ya rangi ya lesi, shati la michezo lenye rangi za kijani na bluu na mashuka mazuri ya pamba yanaonyeshwa na Amina katika duka lake dogo la nguo za mitumba katika barabara ya Uwanja wa Ndege, zote zikiwa zimefuliwa vizuri, kupigwa pasi na kutundikwa katika henga. “Ninapata wateja matajiri na maskini”, anasema kwa tabasamu, “kutoka kwa meneja hadi kwa katibu muhtasi.” Marobota ya nguo za mitumba pia yanaweza kupatikana katika eneo la soko la Mwanakeregwe; hata hivyo, tofauti na mathalan nguo maarufu za mitumba zilizochaguliwa kwa umakini katika soko la Moshi, Tanzania bara, hapa Mwanakeregwe ni sehemu ya vumbi na yenye pilika pilika nyingi, kwa hiyo manunuzi hapa yanaweza kuwa magumu. Kwa hiyo, ningependelea kufanya manunuzi katika maduka madogo kama duka la Amina na maduka makubwa kama la Bi Aziza (angalia kijisanduku kupata anwani) na dakika tano baadaye namiliki blauzi ya lesi kutoka duka la Amina kwa shilingi TZS 10.000.

SANDUKU(BOX)

Maduka ya Vitu vya Mitumba

  • Said Suleiman Mohammed anaweza kuombwa kuongoza ziara za manunuzi katika maduka. Said mwenye umri wa miaka 50, mwongozaji wetu katika maeneo- ni mtaalamu wa miti shamba na mwongoza ziara; anafanya ziara kutoka shamba la viungo hadi eneo la maduka ya nguo za mitumba. Wasiliana kwa namba ya Simu /whatsapp: +255 777 415 558
  • Duka la Bi Azizala Vifaa vilivyotumika vya umeme, majokofu, majiko, vifaa vya mapishi & vingine vingi zaidi. Lipo barabara ya Mombasa. Wasiliana kwa namba +255 777 417 457
  • Duka la Mahmoud la samani za Misri, lina karibu kila kitu, lipo eneo la Magomeni, Wasiliana kwa simu namba +255 777 306 297
  • Duka la Juma la samani za Uingereza, kutoka bidhaa za samani za mitumba hadi nguo za lineni, lipo katika eneo la Saateni, wasiliana kwa namba ya simu ‎+255 714 919 133
Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Fumba Mbili-Wazo Moja

Jua yote kuhusu maendeleo mapya ya bahari ya kusisimua nje kidogo ya mji wa Zanzibar Yote yanafanyika kwenye peninsula ya Fumba: Maendeleo makubwa mawili ya mali isiyohamishika yanaunda nafasi ya kisasa ya kuishi yenye nyumba za likizo na nyumba za kudumu za familia karibu na mji mkuu uliojaa watu. Imeandikwa na ANDREA TAPPER Jumuiya zote mbili zinazotarajia kuwa kando ya bahari, zilianza mwaka wa 2015/16, zinawavutia wenyeji na […]
Soma zaidi
Oktoba 13, 2021
2 dakika.

Ndani ya Fumba Town

Hadithi za kweli za wakazi wapya “Wazanzibari wanajaliana” Mseja na mwanafunzi wa Kiswahili, Sarah Bennet, 27, kutoka Pennsylvania walihamia Fuma Town kwa sababu ni nafuu na salama. Unaonekana kuwa na mwonekano bora zaidi mjini… Ndiyo, kutoka kwenye nyumba yangu ndogo kwenye ghorofa ya pili naweza kuona […]
Soma zaidi
Oktoba 13, 2021
3 dakika.

Nyuma ya pazia

Kuvaa madirisha yako kwa mtindo Nani anaweza kupinga kuchora kwa mapazia? Soma hapa kile ambacho ni maarufu, huzuia joto, mwanga na majirani wanaotamani - na inapatikana Zanzibar na Tanzania. Na Itika Killimbe Drapery inafurahisha. Lakini baadhi ya wakazi katika Mji wa Fumba hawataki mapazia hata kidogo, kwa sababu mbili: ”Mimi […]
Soma zaidi
Septemba 28, 2021
2 dakika.

Tayari shujaa wa kijani kibichi akiwa na miaka 20

"Sio kila mtu lazima asome" anasisitiza Maliha Sumar na kuchagua taaluma tofauti ya kijani badala yake. Maliha Sumar mwenye umri wa miaka 20 tu, ambaye ni mzaliwa wa Tanzania, tayari amefanya sehemu yake ya haki katika kuokoa dunia. Alipigana dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa, alikusanya taka za plastiki, alijiunga na wanaharakati wa boti ya "Flipflopi" huko Mwanza, ambao walisafiri kutoka Lamu nchini Kenya […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

Tunaweza kukusaidia katika kila hatua ya njia

JIFUNZE ZAIDI
Whatsapp Nasi