Oktoba 13, 2021
Dakika 3. Soma

Nyuma ya pazia

Kuweka mapazia katika madirisha yako kimtindo

Nani anaweza kuzuia mpangilio wa mapazia? Soma hapa maana ya mitindo, yanatunza joto, mwanga na kuwazuia watu wanaopenda kuchungulia ndani –na yanapatikana Zanzibar na Tanzania

Na Itika Killimbe

Uwekaji mapazia unafurahisha. Lakini baadhi ya wakazi wa Fumba Town hawapendi kabisa mapazia, kwa sababu mbili: “Napenda kuangalia moja kwa moja hadi baharini kupitia dirisha langu”, anasema Doreen Myers, akiishi kwa furaha katika ghorofa ya tatu ya moja ya majengo. “Wakati wa usiku nafunga madirisha kuzuia watu kuchungulia ndani”, anasema mpangaji mmoja wa nyumba maarufu ya mjini. Hata hivyo kupendelea madirisha yasiyo na mapazia kuna baadhi ya hasara zake: Inaifanya nyumba yako kuwa “tupu” na jua kupiga ndani.

Mapazia yawe ya kawaida au ya gharama, mapazia siyo tu kwa ajili ya kufunika dirisha. “Mapazia yanafanya chumba kipendeze. Yanaongeza ubora na thamani katika nyumba”, anafahamu Katty Harthy, mtaalamu wa ubunifu katika kampuni ya ndani ya Dolson Interiors.Kwa Zaidi ya miaka 15 ukamilishaji wa nyumba jijini Dar es Salaam umetajwa kuwa moja ya kazi za weledi wa juu kufanywa na kampuni za ndani za ubunifu.

“Mapazia ya sebuleni yanafanya nyumba ionekane imekamilika na yenyewe yanakuwa mapambo”, anasema Harthy. “Pia chagua vifaa bora vya kutundikia mapazia katika madirisha yako. Mathalan, kamilisha mapazia yako kwa kutumia vifaa vya kawaida lakini vya kisasa, au vifaa vya asili na weka ubunifu, na italeta kitu tofauti cha kuvutia.”

Mwelekeo wa matumizi ya mapazia hivi sasa ukoje?

Mwaka 2021, wabunifu wanapendelea malighafi za asili, kama vile hariri na lineni au pamba halisi, pamoja na uchoraji wa asili. Mitindo ya urembo urembo kwa sasa haipewi nafasi labda upende vitu vilivyokakaa kiaina (na kwa nini, ni juu yako!). ‚Biophilic design’ ni neno lingine linalobamba au kushika kasi katika sekta ya ujenzi. Lina maana ya kutengeneza nyumba ambayo inahusiana Zaidi na uasilia (katika hali hiyo tazama kwanza Fumba Town “Home Story” katika Makala ijayo, ambayo itaangazia Zaidi nyumba za kustaajabisha msituni kutoka hapa Zanzibar!) Michoro ya asili kama vile maua, wanyama au michoro ya mianzi ni maarufu na iko katika kundi la ujenzi unaoendana na mazingira ya asili, ‘biophiolic’.

Rangi gani?

Nje ya rangi nyeupe, rangi ya maziwa na kijivu na kahawia iliyopauka ni rangi pendwa. Rangi ya udongo inatumika kwa matumizi mengi. Watanzania kwa sasa wanapendelea rangi ya kijani, anasema Katty Harthy wa kampuni ya Dorson. “Rangi ya kijani iliyokoza au kijani kibichi ni rangi zinazokimbiliwa”, anaeleza, „ zinakimbiliwa.” 

Kipimo cha urefu kwa pazia ni kipi?

Wakati kwa sasa ni mtindo kwa pazia kuwa refu na kugusa sakafu au kuwa refu Zaidi, wataalamu wanapendekeza kuwa pazia ining’inie nusu inchi ( ½ inch ) juu ya sakafu ili kuweka urahisi wa kutundika kwa kufanya hivyo pia kunaruhusu kazi za usafi wa sakafu kufanyika bila usumbufu.

Namna ya kupima ikoje?

Pima upana wa ufito au dirisha kutoka kushoto kwenda kulia. Sheria ya msingi inasema mapazia yanatakiwa kuwa mara mbili ya upana wa dirisha lako ili kupata mwonekano wa upana sahihi. 

Vibati au mapazia?

Kuamua kuhusu kutumia mapazia au mapazia ya vibati inategemea na kilicho chini ya dirisha. Dawati au kitanda? Hivyo uwekaji wa pazia ni muhimu. Madirisha membamba, marefu au madirisha madogo ya jikoni nayo yanatakiwa kupambwa. 

Kitu gani kinazuia jua kwa ufanisi?

Mapazia mazito na mapazia ya kuleta kiza chumbani ni chaguo zuri mbadala. Mapazia yenye uzi mrefu zaidi yana kawaida ya kuzuia miali ya jua vizuri zaidi.

Gharama za kutengeneza pazia?

Kwanza chagua kati ya mapazia yanashoneshwa kwa mahitaji ya mteja au yaliyokwisha shoneshwa, yaliyokwisha shoneshwa bila shaka gharama yake ni rahisi kuliko hayo mengine. Pia kanga zikipimwa na kushonwa vizuri pamoja zinaweza kutumika kama mapazia mbadala na yanayopitisha hewa. Ziweke katika jozi kwa lengo hilo. Mama zetu bado wanaamini kuwa pazia lenye thamani lazima liwe na kitambaa cha lineni ndani yake lakini leo unaweza kuwa na pazia bila kitambaa hicho, kwa mfano kwa kuwa na mapazia ya kitambaa cha pamba kinachopitisha mwanga kwa kiasi. Gharama zinatofautiana kutoka dola moja hadi 200 kwa mita kutegemeana na kitambaa, mtindo na uwezo wa mnunuzi. Baadhi ya mapazia ni laini zaidi na ya gharama ya chini; mengine yamekuwa mazito Zaidi na yanapendeza. Kitambaa kinavyokuwa kizito zaidi, ndivyo gharama yake inavyokuwa juu. Pia fikiria kuhusu fito za kutundikia mapazia. Baadhi zimetengenezwa kubeba mapazia makubwa, mazito yanayostahimili kubeba uzito mkubwa, baadhi ya fito zinaweza kubeba mapazia kadha katika ufito mmoja.

TUMA au WEKA MAONI MWISHONI:

Manunuzi kwa mapambo

  • Mambo ya Ndani ya Dolson

3 Chole Road, Masaki, Dar es Salaam

[email protected]

+255 684 911 111

www.dolsoninteriors.com

Mapazia ya aina zote, karatasi za ukutani, na mali ghafi nyingine za mapambo ya ndani – mchango wa mteja ni pamoja na kutembelea maeneo, kuchukua vipimo na kushona kwa gharama ya dola $100.

  • Duka la Suma-Suma General Store

Darajani, Zanzibar

Duka la vitambaa mbalimbali vya nguo (Wide range of fabrics)

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Fumba Mbili-Wazo Moja

Find out all about new exciting seaside developments just outside Zanzibar city It’s all happening on the Fumba peninsula: Two major real estate developments creating modern living space with holiday flats and permanent family homes near the overcrowded capital. By ANDREA TAPPER Both aspiring seaside communities, started in 2015/16, fascinate locals as well as a […]
Soma zaidi
Aprili 15, 2024
3 dakika.

"ZANZIBAR IS SO SUBLIME"

The son of Femi Kuti and grandson of Fela Kuti headlined one of the best Busara festivals ever By Andrea Tapper  He flew into Zanzibar, capturing the hearts of music fans from all over. Afrobeat musician Mádé Kuti, 28, and his wife Inedoye, 25, made time for an exclusive interview with THE FUMBA TIMES before […]
Soma zaidi
Aprili 12, 2024
2 dakika.

MANHATTAN MEETS FUMBA

Manhattan is 14.6 kilometres long and 3.5 km wide. Fumba is 14.3 kilometres long and 3.6 km wide. Otherwise, the two peninsulas couldn’t be more different, of course. Glitzy Manhattan, one of the commercial and cultural centres of the world, full of skyscrapers, banks, offices, residential skyscrapers. Fumba in Zanzibar, still green and rural, showing […]
Soma zaidi
Aprili 8, 2024
4 dakika.

HAS THE WEATHER GONE CRAZY?

EXCLUSIVE INTERVIEW Incredible heat, endless rains – has the weather gone crazy? THE FUMBA TIMES editor-in-chief Andrea Tapper asked a man who knows a lot about the climate in Zanzibar: Hassan Khatib Ame, 44, head meteorologist at the international airport. THE FUMBA TIMES: Am I wrong, or has it been even hotter and more humid […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

25 essential questions and answers to buy property in Zanzibar

READ MORE
Whatsapp Nasi