Agosti 3, 2021
Dakika 3. Soma

Wameowa hivi karibuni. Just Married!

Hakuna kinachozidi harusi katika fukwe za kitropiki. Sherehe ya XL- yenye vionjo vya mahaba, mwanga wa jua ni wa uhakika. Soma hapa, sababu ya Zanzibar kuwa mahali pa sherehe za ndoa ni muujiza. Gundua siri za desturi ya ndoa za Kiislamu na siri ya uzuri wa Afrika kwa siku yako kuu katika maisha yako.

Pamela anakumbuka harusi ya Liz na Marc kana kwamba imefanyika jana. Watu wa mchanganyiko halisi, Liz anatoka Marekani, Marc anatoka Lebanon, wakiishi Tokyo. Liz alipanda mlima Kilimanjaro pamoja na dada yake kabla ya siku hiyo kubwa. Badala ya kuoga harusi alikuwa na wanawake waliojawa furaha wakikusanyika katika Klabu ya Upendo ya Ufukweni.- Baadaye akafika Khaled na Emily kutoka Dubai, maharusi wengine, harusi tofauti kabisa. Wawili hao walisafiri kwenda Zanzibar kuvalishana pete za harusi “Siku ya harusi, nilikutana nao wakirudi kutoka kuogelea bahari ya Hindi”, Anakumbuka Pam Matthews. “Walikuwa wamelowa chapa chapa, harusi ilifana”

Pamela Matthews, 47, ni mmoja wa waandaji harusi maarufu kisiwani Zanzibar “Baada ya kuondoka kutoka Uingereza kuja Zanzibar miaka kumi iliyopita, na kuwa na kisiwa changu hapa cha kufanyia harusi, bado nakipenda kisiwa hiki kizuri“, anasema. Akiwa ameandaa zaidi ya harusi 24 za kimataifa akiwa na kampuni yake ya Castaway Weddings, anajua changamoto (“anamalizia baada ya kutengeneza nywele kwa $200!”) na sifa (“familia yako na marafiki watapapenda hapa”). Anaandaa sherehe kali kwa mamia ya wageni na kupanga matukio kadha ya karibu na wanandoa tu. “Pia tunatafuta mashuhuda wa ndoa, iwapo ni lazima”, anathibitisha Pamela. Msajili Mohammed Kally, 43, mmoja wa wafungisha ndoa rasmi watatu wa serikali mjini Zanzibar, anaahidi: “Tunasafiri kwenda popote wana ndoa wanapopenda kufungia ndoa yao.” Changamoto kubwa kuliko zote mpaka sasa ni nini? “Hakika ni ndoa za ukingo wa mchanga”, anasema, “kuvuka kwa boti kunaweza kuwa kwa kuogofya. Tumejifunza kubaki na vyeti vya ndoa hata kama kuna shida gani” Gharama ya kuandikisha ndoa ni dola $450, kisiwani Zanzibar kiasi hicho kinaonekana kuwa kikubwa sana lakini kinahusishwa katika mchakato mrefu wa ndoa.

Kwa mshangao, ndoa za mbali zina gharama ndogo kuliko zinazofanyikia nyumbani.“Wageni wanalipia wenyewe sehemu ya gharama, kama tiketi na hoteli”, anaelezea mratibu wa shughuli Pamela. Wakirejea maharusi wanaelezea “uzoefu”: chakula cha mchana mara baada ya kuwasili, safari za boti zinazofanyika siku moja baada ya tukio. Fungate linajumuishwa wakati maharusi wanaendelea na ndoto ya mapumziko baada ya kuwekeana nadhiri – muunganiko huu huitwa “mwezi wa harusi”. Harusi za Zanzibar ni maarufu kwa maharusi wenye umri kati ya miaka 25-55; “wazee mara nyingi wanawaleta watoto wao” anasema Pamela. Utaalamu wa kiutamaduni kama vile kupakaa henna kwa bibi harusi(angalia taarifa katika ukurasa unaofuata) au maeneo kama makazi ya zamani ya Sultan yanapendwa mno. 

“Matarajio makubwa yanaweza kuwa changamoto”, anaelewa Ash, 29, mpiga picha wa eneo hilo ambaye amepiga picha za Wamasai katika ukurasa huu. “Kila wanandoa wanataka muda huu kuwa wa kipekee, wakati mwingine huwa wanashangaa, kwa nini kuna watu ufukweni. Lakini ufukwe ni eneo la wazi la umma kisiwani Zanzibar!” Ameandaa kichekesho cha kuchangamsha moyo kutoka mfadhaiko wa mapenzi: “Jifanye kupendana.” Hata corona haikuweza kuvunja hamu ya harusi katika Zanzibar. Wanandoa kadha kutoka Poland walifunga ndoa katika hoteli ya Pili Pili wakati wa janga la corona. “Upendo haufutwi”, mmoja wa wana ndoa alibainisha kwa furaha. Mpiga picha wa Stone Town Robin Batista, 45, ambaye amepiga picha zaidi ya 500 za harusi katika kipindi cha miaka 16, anasema baadhi ya wanandoa wake wanarudi kufanya sherehe: “Tumekuwa marafiki.”

Bahamas, Hawaii, Jamaica, Mexico na …. Zanzibar!Katika miaka mingi iliyopita kisiwa hiki cha Kiafrika kimejipenyeza na kuingia katika madaraja ya maeneo yanayovutia kwa shughuli za harusi. Utamaduni mahiri, watu wapole, fukwe nzuri na hoteli, makazi ya zamani ya kisultani na mapishi mazuri ya chakula ni mambo yanayokifanya kisiwa cha marashi ya karafuu kuwa sehemu ya kipekee ya shughuli za harusi. “Fukia miguu katika mchanga na mtu wa karibu yako kabisa na mpenzi wako mkubwa akiwa karibu yako”, anasema Pamela Matthews ambaye bado anapenda kazi yake, “unahisi upendo, inafurahisha.” 

Ukirudi nyuma katika miaka ya 1960, maeneo ya shughuli za harusi yalijulikana (na yalipendwa) kwa mwonekano wake na uzuri wa asili. Baada ya miaka mingi kupita, yametoka kwenye mwendelezo kuwa maeneo makuu ya shughuli za harusi. Kila mwaka kuna karibu maeneo laki tano ya harusi duniani kote kwa mujibu wa tovuti ya destinationweddings.com.

Harusi za Castaway zinazaanzia dola 2500$. „Kwa kituo cha harusi, utatakiwa kushauriana faida“, jarida la ushauri wa wanawake la Harper’s Bazaar - „Endapo tu ni kuepuka saa 250 ambazo wanandoa kwa wastani wanatumia katika kupanga harusi“, anasema Pamela Matthews. Muda wa maandalizi muhimu ni miezi mitatu hadi sita. Maharusi wa Kikorea walipeana maua ya waridi katika harusi ya kupendeza. “Kaptula kwa bwana harusi ni mavazi yanayokubalika”, anasema Pamela. Kuvaa kwa kupendeza au rasmi kama unavyohitaji kuwa, harusi katika ufukwe wa kitropiki ni simulizi za kweli.

Maelezo zaidi:

Castawayweddings.com

Theknot.com

Marthastewart.com

Harusi:

131 

Wastani wa hesabu ya wageni nyumbani

30   

Wastani wa hesabu ya wageni katika harusi ya kitalii

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Fumba Mbili-Wazo Moja

Find out all about new exciting seaside developments just outside Zanzibar city It’s all happening on the Fumba peninsula: Two major real estate developments creating modern living space with holiday flats and permanent family homes near the overcrowded capital. By ANDREA TAPPER Both aspiring seaside communities, started in 2015/16, fascinate locals as well as a […]
Soma zaidi
Mei 6, 2024
3 dakika.

THE NEW BAGAMOYO CONNECTION

Revisiting colonial routes. For the first time, a water taxi connects Stone Town with the coastal heritage town Bagamoyo on the mainland. The trip takes about one hour. For tourists and residents, it opens up an excursion into the past. The endeavour is the brainchild of Joanna Turner, a cultural entrepreneur and daughter of a […]
Soma zaidi
Mei 2, 2024
3 dakika.

HOW TO RUN A SUCCESSFUL AIRBNB

In Fumba Town and elsewhere in Zanzibar In 2012, Airbnb listed three apartments in Zanzibar. Today, more than 1,000 holiday apartments and villas are found on the isles: from a shipping container in Paje to a tree house in Bwejuu. Two popular Airbnb hosts in Fumba explain what works best – for them and their […]
Soma zaidi
Aprili 22, 2024
2 dakika.

STREET NAME COMPETITION

Living on Opportunity Lane. Let’s give our streets names! Fumba Town is growing, looking for a name concept for its streets, alleys and pedestrian lanes fitting a cosmopolitan, nature-loving community. Send us your ideas!Have you experienced this? You order take-away, and the piki driver calls you five times asking for directions before he finally stands […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

25 essential questions and answers to buy property in Zanzibar

READ MORE
Whatsapp Nasi