Septemba 10, 2021
Dakika 4. Soma

Fumba ni kwa kila mtu (Fumba For Everybody)

Makazi mazuri kwa gharama nafuu katika Fumba Town – Nyumba ndogo hukodishwa kuanzia $150

Na Andrea Tapper

Kuishi kwenye mwanga ni msemo mpya Zanzibar. Nyumba zenye bei nafuu zinauzwa. Panga katika mazingira safi na salama yakivutia watu wengi zaidi katika Fumba Town iliyoko kando ya bahari.

Sharmim Esmail meneja wa mji huo anafahamu kila sentimeta ya ardhi ni muhimu katika nyumba yenye eneo la mita za mraba 21. Na zaidi ya hapo nyumba hiyo imekamilishwa kwa samani nzuri ikiwekewa kitanda kikubwa kilichotengenezwa kwa mbao za mnazi ikiendana na sofa lenye rangi za kuvutia za kiafrika, meza ya chakula ya watu wawili, kabati la nguo na sehemu ya kusomea. Nyumba ndogo za kupanga Fumba Town zinakwisha haraka kuliko zinazojengwa. Akikagua droo za nguo katika kitanda na sofa, muuguzi Rachel 28 anaonekana kufurahia nyumba anayotaraji kuimiliki na ndivyo ilivyokuwa kwa Omar 27 wakati mauzo kwa mtu anayetaka kuishi Zanzibar angalau kwa miaka miwili.’’Hii hakika ndiyo nyumba niliyokuwa nikiitafuta.’’ Anasema’’ Simu yake ya mkononi ikiita mara kwa mara ni wazi kuwa ni mtu aliye na shughuli nyingi.

Kuanzia dola $150 kupanga nyumba ndogo zinafaa vijana ambao ni wateja wa baadaye wa nyumba za Fumba Town. “Fumba Town si kwa wageni na watu matajiri pekee” anasisitiza Tobias Dietzald, Afisa Mkuu uendeshaji,COO wa kampuni ya CPS, mwendelezaji wa Kijerumani aliye mhimili wa mradi huu, “Tunaendelea kupanua kazi zetu ili kuwezesha sehemu kubwa zaidi ya jamii inafurahia maisha ya Fumba..” nyumba 900 za makazi zimeuzwa, zinakaliwa au ziko kwenye hatua ya ujenzi. Hatimaye ndoto ya mji wa kijani itakuwa na nyumba za makazi 3000, kutoka nyumba za ghorofa hadi nyumba za kawaida za mjini na nyumba kubwa za kifahari. Nyumba ya kwanza ilikabidhiwa mwaka 2018. 

Kila inchi na kona ya nyumba ndogo za Fumba-inapatikana pia nyumba zisizokamilika- zimepangiliwa kwa umakini mkubwa kwa kujengewa nafasi ya stoo. Sehemu ya jiko karibu na mlango wa kuingia ndani pamewekwa jiko lenye sehemu ya kuokea, sahani mbili za jiko na jokofu; bafu lenye kusakafiwa kwa marumaru pamoja na bomba la maji ya kuoga na sehemu ya msalani inatoa nafasi kubwa kuhifadhi vitu vya kutumia maliwatoni na taulo zikitundikwa katika ukuta wa mbao. “Nyumba hiyo inafaa kwa mtu mmoja”, anaeleza meneja wa mji Esmail, “kwa wanataaluma vijana au wanafunzi. Kutokana na kuwa na pilika nyingi siku nzima, wanahitaji sehemu nzuri na salama ili kupumzika usiku. Jokofu iliyopo ni kubwa kuliko ya kwenye chumba cha hoteli; unaweza kuandaa chakula cha kawaida katika jiko lako na baadaye kupumzika katika sehemu yako binafsi.”

Dhana ya kuishi katika nafasi yenye starehe kwa gharama nafuu ni dhana mpya kwa Zanzibar, hata kwa Afrika Mashariki. Nyumba za Fumba ni sehemu na kifurushi cha miundombinu ya kisasa ya hali ya juu ikiwa na mtandao wa internet wa Wifi wenye kasi ya juu, bustani za kilimo hai, uchakataji wa taka, maji safi ya kunywa na usalama wa muda wote (24/7). Minazi mirefu na miti mingine kama moringa, majengo matano yenye rangi nyeupe yaking’aa yakiwa na roshani na madirisha makubwa yanaonekana kiuhalisia wakati watalii wanapokaribia Fumba Town karibu na kijiji cha Nyamanzi. Nyumba za upande wa bahari zimesambaa katika eneo la ekari 160 la pwani ya bahari ya Hindi kilomita 18 tu kusini magharibi mwa mji wa Zanzibar na umbali wa kilomita 15 kutoka uwanja wa ndege. 

“Miaka mitano iliyopita hayo yote yalikuwa ndoto tu, dira iliyowekwa katika maandishi”, anasema mmoja wa waendelezaji wakuu wa mradi, Tobias Dietzold. Kwa sasa kuna shule, kliniki inayotoa huduma kikamilifu, uwanja wa michezo hata wakati wa usiku, madirisha mengi katika majengo mapya yamewashwa taa. Wakati wa mchana mtu anaweza kuwaona wamiliki wa nyumba wakiendesha magari aina ya pick up, yakiwa yamebeba majokofu, magodoro na vifuniko vya taa. Kila jengo la ghorofa nne katika Fumba Town, lina nyumba kati ya 16 na 24. Majengo mengine tisa zaidi tayari yako katika hatua ya ujenzi na kufanya jumla ya nyumba mpya za kuishi 300 zinatarajiwa. “Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka, tutaleta nyumba ndogo 50 maarufu kama studio kwa ajili ya kupanga”, anasema mwendelezaji wa mji Tobias Dietzold, “juu ya hilo tutakuwa na nyumba za chumba kimoja cha kulala na nyumba za vyumba viwili vya kulala.” Nyumba zote Fumba Town zinamilikiwa na watu binafsi; wamiliki wanaweza kuzikamilisha na kupangisha nyumba zao wakisaidiwa na mpango wa ukodishaji nyumba unaosimamiwa na mji (angalia kisanduku). 

 “Tangu mwanzo ilikuwa wazo letu la kuwa na eneo la kuishi kwa makundi yote ya watu wa vipato mbalimbali”, anasema Sebastian Dietzold ambaye kwa kushirikiana na mke wake Katrin na kaka yake Tobias walianzisha Fumba Town. “Ni kweli, si kila nyumba itakuwa mbele ya bahari, lakini zote zina miundombinu sawa ya kustarehesha”, anaongeza Tobias Dietzold. Kaka hao wawili ambao wamekulia Tanzania, wameahidi: “Tutaifungua Fumba Town hata kuzidi bado tukiwa na dhana ya kujenga nyumba zenye gharama nafuu.” 

Wakati huo huo, baada ya kutengeneza kahawa yake ya kwanza katika nyumba yake ndogo na kufurahia mandhari ya bahari,mpangaji Rachel ana swali moja zaidi: “Itakuwa salama kwangu nikirejea usiku?” Meneja wa mji Sharmin Esmail hasiti kumhakikishia: “Ukiwa mwanamke unayeishi peke yako mwenyewe naelewa umuhimu wa usalama. Kwa kuwa na kamera za ulinzi maarufu kama CCTV na walinzi wa doria, Fumba Town kila hatua unayopiga kutoka nyumbani na kurejea ni salama.”

Maswali matatu kwa meneja wa mji Sharmin Esmail kuhusu faida ya Fumba Town: 3 questions to the town manager

Sharmin Esmail about the advantages of Fumba Town:

.

Naweza kupanga nini? Kwa nyumba zaidi zinavyoendelea kujengwa na kukamilishwa, wapangaji wapya wanaingia sokoni karibu kila siku, miongoni mwao nyumba ndogo 50 zimekamilika au zinaendelea kukamilishwa, nyumba za chumba kimoja na vyumba viwili vya kulala na nyumba za mjini zenye vyumba hata vitano vya kulala zinapatikana. Fumba Town ni mji mpya wa ufukwe wa bahari, ni mwendo wa dakika 20 kwa gari kutoka mjini Zanzibar. Tunakupa maisha ya hali ya juu kwa miundombinu mizuri kwa kila mtu kulingana na kipato chake. Na tuna machweo mazuri ya jua hapa!

Gharama ya pango ni kiasi gani - How much is the rent? 

Nyumba za studio zinaanzia $150, nyumba zenye chumba kimoja cha kulala zinaanzia dola $250, nyumba za vyumba viwili zinapatikana kwa gharama ya kuanzia dola $350. Nyumba za mjini zenye vyumba 2-5 vya kulala zinaanzia dola $450. 

Naweza pia kununua nyumba kulingana na bajeti yangu? Mtu yeyote mwenyeji au mgeni, anaweza kununua nyumba Fumba Town kwa umiliki ardhi wa miaka 99. Bei inaanzia chini kiasi cha dola $25,900 kwa nyumba ndogo na kupanda juu kufikia dola 300.000 na zaidi kwa nyumba kubwa. Zaidi ya nyumba 900 zimeuzwa kama za uwekezaji, nyumba za shughuli za kitalii au makazi ya kudumu. Tunatoa huduma za ukamilishaji wa nyumba na bei za kupangisha kwa wamiliki wa nyumba.

Maelezo-Information: fumba.town, Tel.255 623 989 900

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Two Fumbas – One Idea

Find out all about new exciting seaside developments just outside Zanzibar city It’s all happening on the Fumba peninsula: Two major real estate developments creating modern living space with holiday flats and permanent family homes near the overcrowded capital. By ANDREA TAPPER Both aspiring seaside communities, started in 2015/16, fascinate locals as well as a […]
Soma zaidi
Oktoba 23, 2023
2 dakika.

The unknown side of Zanzibar

Location Most secluded in Zanzibar, The Bottom Line Feel like a VIP by the ocean The road maybe rocky, but the destination rewards us for travelling it. Like a Fata Morgana, white modern villas suddenly become visible high above the sea, a wooden deck with neatly arranged cabana-like double sun beds leads to an endless […]
Soma zaidi
Oktoba 17, 2023
2 dakika.

FAKE Picture – OR NOT?

By Elias Kamau A tree house in Stone Town? Too good to be true! When we received this photo at THE FUMBA TIMES, we became highly sceptical. Here’s a guide to help you recognise fake shots – especially in your social media.  The commonsense warning is clear: don’t believe everything your Facebook and Instagram friends […]
Soma zaidi
Oktoba 3, 2023
2 dakika.

LET THE SUNSHINE IN

A German couple, one of the first buyers of a beach front house in Fumba Town, wants to start a solar business here. Engineer Ronny Paul, 44, produces custom made solar systems.  There seems to be good news on the solar front: a first photovoltaic project is planned for Bambi in the heart of the […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

25 essential questions and answers to buy property in Zanzibar

READ MORE
Whatsapp Nasi