Septemba 16, 2021
Dakika 4. Soma

Hazina iliyopotea? (Treasures Lost?)

Magofu ya kihistoria ya Mtoni na Mbweni yakiwa njia panda

Zanzibar ina utajiri mkubwa wa urithi wa utamaduni- ambao ni kivutio kikubwa cha utalii. Lakini mpaka sasa kisiwa hiki kimeonyesha nia ya kuuhifadhi utamaduni huu. Magofu mawili nje kidogo ya mji kwa sasa yanasubiri wakati mzuri zaidi kushughulikiwa.

Saleh Mohammed amekaa nyuma ya meza kukuu ya mbao katika kivuli cha mwembe, vipeperushi kadha kuhusu „taa za mishumaa wakati wa chajio (chakula cha usiku)“ na „safari za kitalii maeneo ya kihistoria“ vikiwa mbele yake. Lakini hapajawa na chajio kwa miaka mingi. Wala hapajawa na watalii. Tunamwuliza, 31, kwa mara ya mwisho ni lini watalii walitembelea magofu ya Mtoni, mabaki ya thamani ya kale kuliko yote ya kasri kubwa kuliko zote za Sultan kisiwani Zanzibar. „Hakuna watalii leo, wiki iliyopita na mwezi uliopita pia hapakuwa na watalii“, mwongoza watalii huyo ambaye amekosa kazi alijibu kinyonge. Hali hii inaonekana ngeni, ili hali magofu ya kasri yako karibu na hoteli ya kitalii, Hotel Verde, kiasi cha umbali wa kilomita tano kaskazini mwa mji wa Zanzinzibar. Lakini sehemu hii ya kitalii isiyo na vileo inaonekana kuwa na vipaumbele vingine kama utalii wa michezo ya baharini. Ikijengwa katika bahari dhidi ya tahadhari za wanamazingira, takataka za plastiki hazikuweza kuhimili mawimbi na upepo; njia mbadala katika maegesho pia kwa sasa haifanyi kazi.

Mbweni

shule ya wasichana watumwa walioachiwa huru

Picha tofauti inajieleza kwetu katika vitongoji vya kusini mwa mji wa Zanzibar, yaliko magofu ya Mbweni, mabaki tete ya nyumba ya zamani ya watawa na katika karne ya 19 nyumba hiyo iligeuzwa kuwa shule ya wasichana waliokolewa kutoka utumwani, wakiwa huru, kwa sasa yanajumuishwa katika hoteli mpya, “Jungle Paradise”. Baada ya mabadiliko kadha ya umiliki na miaka mingi ya kutelekezwa kwake, sakafu ya kihistoria kwa sasa imesafishwa na kuwa safi tena; maua yamefunika katika kuta za zamani. “mimea 670 na aina za miti, miongoni mwao aina 200 tofauti za minazi, tunapanga kufungua bustani ya miti na maua hivi karibuni”, anaelezea meneja mpya wa hoteli Christian Rockenbauer, ambaye hivi karibuni amechukua maeneo hayo 

Mmiliki huyo wa kijerumani mwenye umri wa miaka 46 haraka amekarabati njia yenye urefu wa mita 120 inayoelekea katika bahari ya Hindi, amefungua baa mpya inayofunguliwa majira ya jioni na kukarabati mazingira yote yaliyochakaa ya hoteli ya Protea ya zamani, moja ya hoteli chache za upande wa magharibi yenye ufukwe mzuri.

Baada ya shughuli za kazi za Ijumaa, ni wakati kwa klabu ya chakula cha mchana sasa kuwavutia vijana wengi. “Magofu ya Mbweni ni moja ya vivutio vyetu vikubwa,” Chris Rock ananieleza, “bila shaka tutayahusisha katika shughuli mbalimbali; Kanisa la zamani litatumika kwa shughuli za harusi.”

Ni wasichana wangapi yatima wamekuwa na ndoto za harusi zao kufanyika mahali hapa, shule ya zamani ya Victoria St. Mary? Waliachiwa huru kutoka majahazi ya watumwa yaliyokuwa yakiwasafirisha kati ya mwaka 1870 na 1900, walifundishwa kuwa walimu, wasusi wa vikapu, washonaji na wapishi. Mwaka 1906 shule hiyo ikijumuisha nyumba ya zamani ya Kiarabu, ikawa nyumba ya watawa. Baadaye jengo hilo la ghorofa mbili likachakaa na kuwa gofu lakini kanisa licha ya kutokuwa na paa, limebaki vile vile na hata limetumika kufundishia madarasa ya yoga muda uliopita.

Kwa nini kasri ya Mtoni imesahaulika?

(Why is Mtoni palace forgotten?)

Kwa upande mwingine kasri ya magofu ya Mtoni, yaliyopo umbali wa kilomita mbili kaskazini mwa Maruhubi, yanaonekana kuhamwa au kutelekezwa, japokuwa magofu hayo yamefunikwa na nyasi zilizoota lakini bado yanaonekana kuvutia: hamamu binafsi kadha, wakati fulani zilileta maji ya chemichemi kutoka mlimani kwenda “Beit il Mtoni” na maeneo ya ndani. Wakati mpiga picha wa jarida la THE FUMBA TIMES Keegan Cheick akirusha drone yake juu ya majengo hayo, mpangilio wa kasri ya zamani ulionekana bayana. „Tulikuwa na kawaida ya kuitunza kasri hiyo, hata kutoa mawazo kwa matumizi ya baadaye ya kasri lenyewe ambayo yote yalikataliwa na serikali. Halafu tukarejesha mnara serikalini mwaka 2018“, Anaeleza meneja Nasheeb Uddin wa hoteli ya inayomilikiwa na Bakhresa, Hotel Verde. 

Kasri hiyo kongwe kuliko zote Zanzibar iliyo katika ufukwe wa bahari ya Hindi, yalikuwa makazi ya Sultan Seyyid Said (1806-1856), akiwa na mke halali mmoja, vimada 75 na watoto 36. Katika siku zake za mafanikio, watu wapatao elfu moja waliishi hapa, miongoni mwao ni binti mdogo wa sultan, Princess Salme ambaye baadaye alipata umaarufu wakati alipotoroka kwenda Ujerumani na mfanyabishara wa Kijerumani. Mvumbuzi Richard Burton aliyaelezea makazi ya kifalme kama nusu kasri yenye mwonekano wa kuvutia. “Muda mwingi wa siku”, Salme pia aliyejulikana kama Emily Ruete aliandika katika shajara yake kutoka mwaka 1886, “tulikuwa tunacheza na tausi au kukaa katika moja ya vyumba vingi vya mvuke katika bafu kubwa.” Baada ya sultan kufa, kasri ilipoteza umuhimu wake. 

Waziri wa Utalii Lela Musaa: “Tunafanya Mtoni kuwa jumba la makumbusho”

 (Tourism minister Lela Mussa:“Will make Mtoni a museum”)

I am meeting the man who knows many historical details about the site and successfully ran it some time as a cultural event spot. Tonino, as everybody calls him, is Italian and a long-time Zanzibar entrepreneur. “Concept? Nobody had a concept!” he indignantly exclaims, when I report my findings at Hotel Verde to him. “All they had planned was to put aluminium windows in the ancient coral palace walls.” That, luckily, didn’t happen – but nothing else either. When contacted by THE FUMBA TIMES, Zanzibar’s new Minister of Tourism and Cultural Heritage, Lela Muhamed Mussa, however now announced: “We are going to revive Mtoni and turn it into a museum”. The restoration would be “part of a bigger cooperation with Oman to restore all major monuments”, the minister said.

Mji wa kihistoria wa Stone Town, unalindwa na UNESCO tangu mwaka 2000, umeshuhudia jitihada nyingi za kuukarabati, lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO limeikosoa vikali Zanzibar kwa kushindwa kusimamia kikamilifu maeneo ya urithi wa utamaduni” mwaka 2016. Mnara mkubwa mjini Zanzibar, Nyumba ya Maajabu ilijengwa mwaka 1883, ilianguka Sikukuu ya Krismasi iliyopita.

Utalii usiosahaulika katika mikokoteni ya kuvutwa na punda

(Nostalgic tours in conkey carts)

Mtoni daima haikusahaulika. Kati ya mwaka 2000 na 2015, magofu hayo yalikuwa na pilika pilika nyingi za watu zikihusishwa na uwepo wa hoteli ya Mtoni Marine, hoteli maarufu kabla ya Hotel Verde. “Tulikuwa na mamia ya matamasha ya Taarab, maonyesho ya mavazi na mihadhara”, anakumbuka Antonio “Tonino” Garau, 56: “Nchini Italia utamaduni unaendesha utalii, tulifanya vivyo hivyo hapa Zanzibar.” Stefanie Schoetz,mmiliki wa Kiholanzi wa Duka la urembo la kijadi, aliwatembeza watalii wakiwa katika mkokoteni ulioezekwa makuti ukivutwa na punda wakati wa ziara ya utalii ya kukumbukwa katika barabara za Princess Salme. Alihusika pia katika rasimu ya kurasa 28 za usanifu majengo za Uholanzi “Mchoro wa maisha ya baadaye” Mtoni. Lakini kwa namna fulani mpango huo ulikufa “ Unahitaji mwekezaji mwenye uelewa wa shughuli hizo”, Tonino anahitimisha maelezo yake kuhusu magofu ya Mtoni.

”Ni muhimu kwa Zanzibar kutunza vitu bainifu vyao vya kale”, wana historia wanaunga mkono maoni hayo katika kitabu cha picha, ambacho kimehaririwa kwa pamoja na wana taaluma hao, kikiitwa “Mtoni” (2010). Kinaweza kikatumainiwa kupeleka ujumbe wa kuwaamsha wanasiasa na wawekezaji wa leo kabla ya kuacha kitu chochote cha urithi wa kale.

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Two Fumbas – One Idea

Find out all about new exciting seaside developments just outside Zanzibar city It’s all happening on the Fumba peninsula: Two major real estate developments creating modern living space with holiday flats and permanent family homes near the overcrowded capital. By ANDREA TAPPER Both aspiring seaside communities, started in 2015/16, fascinate locals as well as a […]
Soma zaidi
Oktoba 23, 2023
2 dakika.

The unknown side of Zanzibar

Location Most secluded in Zanzibar, The Bottom Line Feel like a VIP by the ocean The road maybe rocky, but the destination rewards us for travelling it. Like a Fata Morgana, white modern villas suddenly become visible high above the sea, a wooden deck with neatly arranged cabana-like double sun beds leads to an endless […]
Soma zaidi
Oktoba 17, 2023
2 dakika.

FAKE Picture – OR NOT?

By Elias Kamau A tree house in Stone Town? Too good to be true! When we received this photo at THE FUMBA TIMES, we became highly sceptical. Here’s a guide to help you recognise fake shots – especially in your social media.  The commonsense warning is clear: don’t believe everything your Facebook and Instagram friends […]
Soma zaidi
Oktoba 3, 2023
2 dakika.

LET THE SUNSHINE IN

A German couple, one of the first buyers of a beach front house in Fumba Town, wants to start a solar business here. Engineer Ronny Paul, 44, produces custom made solar systems.  There seems to be good news on the solar front: a first photovoltaic project is planned for Bambi in the heart of the […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

25 essential questions and answers to buy property in Zanzibar

READ MORE
Whatsapp Nasi