Juni 16, 2021
Dakika 3. Soma

Kupenda Utamaduni

Tukio la siku tatu, sherehe ya nikah katika msikiti na mavazi ya kuvutia yasiyobadilika kamwe - hii, kiuhalisia ni harusi ya kijadi ya Zanzibar. Stupid simba no

Ndoa za Kiisla mara nyingi zinakuwa na vitu vingi vya kuvutia, ikiwemo tamaduni za kushangaza na matambiko. Matambiko haya yamesambaa, na kuwekwa katika makundi matatu: kabla ya ndoa, wakati wa ndoa na baada ya ndoa. Japokuwa inaonekana kama ni jambo rasmi, sherehe ya Kiislamu kwa kweli ni moja na ndoa zinazofurahisha sana na zenye mvuto duniani. Gharama inatumika kuhakikisha tukio hilo linabaki katika kumbukumbu ya Bibi na Bwana harus, na kwa familia zao na wageni waalikwa. Mtu anaweza kuona mavazi mazuri ya harusi yaliyodariziwa kwa mkono na mitindo mizuri ya urembo. Chakula ni kitamu kikiwa na ladha na harufu nzuri - lakini kwa kiasi kikubwa katika harusi za Zanzibar unaweza kukosa champagne yenye kileo!

Kwa nini wanaume na wanawake wanajitenga katika kusherehekea?

Sherehe za harusi za Kiislamu zinakuwa na baadhi ya taratibu za kuwatenga wageni wa kike na wa kiume, lakini kwa viwango tofauti. Kunakuwa na vyumba vilivyotengwa kwa ajili ya wanaume na wanawake kusherehekea harusi, mgawanyo unaofanywa katika eneo la shughuli, au wanaume na wanawake wanaweza kuwekwa katika makundi katika meza tofauti. “Mwingiliano kati ya jinsia kwa ujumla unazuiliwa”, anasema Faridi Hemed, mwandishi na mtaalamu wa utamaduni kutoka Zanzibar. “Lakini tangu wanaume na wanawake wanachangamana kikawaida miongoni mwao, kila jinsia inahisi kuwa huru kwa kufanya hivyo.”, anasisitiza Faridi. Akizungumza kwa kejeli kiasi anawashauri wageni kutoka nchi za magharibi aliowaalika katika harusi: “Huenda mkahitaji kujifunza upya mtazamo wenu ili kuwa na marafiki wapya katika dansi la shughuli.” 

Gharama zikoje?

Mume wa Kiislamu anatakiwa kukubaliana mahari na mke mtarajiwa kabla ya ndoa. Mara nyingi ni fedha inayotolewa kwa mkupuo ambayo bi harusi anaamua kulipwa kama mahari. Au anaweza kuomba safari, dhahabu au kitu chochote anachotaka. Mahari ni ishara ya uwajibikaji wa mwanaume wa kumtunza mke wake. Iwapo bibi harusi baadaye atataka talaka bila idhini ya mume, anarejesha fedha kwa mume na kuomba apewe talaka ijulikanayo kama khul. Endapo wote wawili watataka kutalikiana au mume pekee, mke anabaki na fedha iliyotolewa kwake kama mahari. “Wastani wa gharama katika harusi za Zanzibar ni kati ya ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu, sawa na dolaza Kimarekani $500-$1500”, anakadiria Faridi, lakini katika harusi nyingine za familia tajiri, gharama zinapanda hadi dola $3000 na zaidi. Mahari huenda ikawa asilimia 60 ya bajeti ya harusi.

Je, harusi za kijadi bado zinapangwa?

Kwa Faridi Hemed, ni swali gumu. Ndoa za Zanzibar bado zinaendelea kupangwa na wazazi, anasema, ambao huenda wanawaelewa zaidi watoto wao.Kwa upande mwingine, mtaalamu huyo anasema, “ndoa inayopangwa ni kinyume cha dini, unatakiwa kuwa katika upendo.” Angalau, Faridi anasisitiza, ndoa lazima yawe matakwa ya wanaooana, na lazima waweze kuwakataa wachumba wao bila kuwaumiza. Katika hali yoyote: Pia, nyakati zinabadilika Zanzibar. Mmoja pekee anatakiwa kumtazama mmoja ambaye wamechukuana naye kwenda eneo la makutano ya vijana katika bustani ya Forodhani, kutambua kuwa tayari wana uhuru mkononi mwao wa kufahamiana kwa karibu.

Nikah ni nini?

Nikah – Tukio kubwa katika ndoa ya Kiislamu– ni sherehe ndogo inayofanyika mbele ya Imam. Mashahidi wawili wanakuwepo, kama ilivyo kwa ndoa ya Kiserikali na Kikristo. Kwa kawaida, sherehe inakuwa na kisomo kutoka Qur'an, na wanandoa kubadilishana viapo. Shughuli inayofuata Zanzibar mara nyingi ni nzuri, sherehe ya hiyari ambako utamaduni unachukua nafasi yake; au, shughuli ndogo zaidi lakini mkusanyiko rasmi wa watu katika ukumbi wa familia ambako nusu ya wanakijiji wanaalikwa na wageni kupewa chakula watakachorudi nacho makwao. Wanandoa wanajitambulisha wenyewe kwa marafiki na familia katika jukwaa lililoandaliwa. Familia tajiri zaidi zinaandaa sherehe ya chakula cha mchana au usiku katika maeneo tofauti tofauti kwa siku tatu. Sherehe za kabla ya nikah zinasherehekewa kwa siku moja au mbili kabla ya tukio kubwa miongoni mwa wanawake nyumbani kwa familia ya bi harusi, na kwa mwanaume nyumbani kwa familia ya bwana harusi- na inaweza kuwa tafrija za wanaume wasiooa na wanawake wasioolewa, zikijaa vituko vingi.

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Fumba Mbili-Wazo Moja

Find out all about new exciting seaside developments just outside Zanzibar city It’s all happening on the Fumba peninsula: Two major real estate developments creating modern living space with holiday flats and permanent family homes near the overcrowded capital. By ANDREA TAPPER Both aspiring seaside communities, started in 2015/16, fascinate locals as well as a […]
Soma zaidi
Aprili 22, 2024
0 mins.

STREET NAME COMPETITION

Soma zaidi
Aprili 15, 2024
3 dakika.

"ZANZIBAR IS SO SUBLIME"

The son of Femi Kuti and grandson of Fela Kuti headlined one of the best Busara festivals ever By Andrea Tapper  He flew into Zanzibar, capturing the hearts of music fans from all over. Afrobeat musician Mádé Kuti, 28, and his wife Inedoye, 25, made time for an exclusive interview with THE FUMBA TIMES before […]
Soma zaidi
Aprili 12, 2024
2 dakika.

MANHATTAN MEETS FUMBA

Manhattan is 14.6 kilometres long and 3.5 km wide. Fumba is 14.3 kilometres long and 3.6 km wide. Otherwise, the two peninsulas couldn’t be more different, of course. Glitzy Manhattan, one of the commercial and cultural centres of the world, full of skyscrapers, banks, offices, residential skyscrapers. Fumba in Zanzibar, still green and rural, showing […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

25 essential questions and answers to buy property in Zanzibar

READ MORE
Whatsapp Nasi