Agosti 9, 2021
Dakika 3. Soma

Kuwa imara katika Fumba (Staying Fit In Fumba)

Mazoezi ya juu ya nyumba ni maarufu New York – na katika Fumba Town. Njoo na ungana na mchezo huu!

Wakati siku ikiishia taratibu kuingia jioni katika Fumba Town, utawaona wakazi wake wakirejea kutoka kazini, kina mama wakiwaita watoto wao kurudi nyumbani kutoka michezo ya nje. Na katika jioni ya siku mbili kwa wiki utapata kundi la watu wakijitokeza kutoka juu ya nyumba moja ya majengo yanayotazamana na bahari. 

Kwa mwonekano wa machweo mengine ya jua likiangaza mwanga wa rangi ya dhahabu katika bahari ya Hindi na sauti za midundo ya kiafrika, kundi hili limekuja kumalizia siku pamoja na “kipindi cha Kundi la Michezo la Fumba”, kinachoongozwa na mkufunzi wa elimu ya mazoezi ya viungo Ahmed Msoma.

 “Watu mara nyingi wanafikiria kuwa nanyanyua uzito, lakini ni kinyume kabisa'', anasema. “ Najifundisha mwenyewe na wateja kwa mazoezi ya viungo. Imarika popote na wakati wowote, hakuna kifaa au gym kinahitajika, hiyo ni falsafa yangu.”

Falsafa hii inathibitisha ukweli huo hususan Fumba, ambako njia zenye miti ya kivuli zinasababisha uendelee kutembea kwa mguu au kuendesha baiskeli. Mji huu umepangiliwa kiasi cha kuwawezesha wakazi wake kutoka nje, kufurahia hewa safi na kutembea huru bila kuhitaji gari. 

Baadhi wanajiunga na madarasa ya ghorofani si tu kwa mazoezi ya uimara wa mwili. “Kwa kujipa changamoto na shughuli tofauti kunafanya akili yangu ichangamke na kunifanya kuwa mbunifu zaidi”, anasema mkazi mmoja. 

Msoma. Mtaalamu wa sanaa za mazoezi ya mwili, anaweza kuwa mtu imara. akili Anajivunia hadhi ya cheo cha sensei na ameshiriki katika mashindano mengi ya kimataifa. Lakini katika madarasa yake hakuna mashindano. “Nataka kumfanya kila mtu kuwa mahiri, bila kujali kiwango cha utimamu wao”, Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 37 anasema. Kwa kuwa mmoja wa wataalam wachache wakufunzi katika kisiwa hiki, ana jambo analolitilia shaka: “Kuongezeka kwa madarasa ya michezo yanakosa uelewa. Fikiria unatoa mafunzo hayo kwa mtu wa aina gani”, anashauri. “Kitu chochote kile hakiwezi kuwa salama.”
Katika mikono yake, katika Fumba, kundi la watu wenye asili na utamaduni tofauti wanahisi kujiamini.“Utaona watu zaidi ya 50 wakitoka jasho kati ya mama mwenye watoto wawili aliyedhamiria na kijana mwenye nguvu tele. Inanipa ufahamu wa maana ya jumuiya kuweza kushiriki darasa kwa pamoja”, mmoja wa washiriki anaeleza.

Msoma pia anatoa mafunzo ya kujilinda kwa wanawake, semina za ofisi na mafunzo binafsi. “Siyo kambi ya buti bali wakati wako”, anawahakikishia wenye mashaka, “afya yako ina thamani ya uwekezaji”. Wakati fursa zaidi za shughuli za michezo zikijitokeza Fumba, Msoma anasisitiza umuhimu wa kutumia fursa yoyote ili kusonga mbele: “Tumia saa za asubuhi tulivu kufurahia matembezi ya amani kupitia mjini, achana na dawati lako kila saa kwa dakika kadha kunyosha mgongo wako. Inaleta utofauti kufikia mwisho wa siku.”

Jiunge na darasa? - Join a class?

Msoma Fitness

Whatsapp: +971 505 610 934

Fumba Sports, Jumatatu na Jumatano saa 12 jioni

Nukuu:

“Afya njema huchangamsha akili yangu” 

“Fitness keeps my brain active”

SANDUKU:

Vitendo bora zaidi kwa kila kizazi

0-18 

Panda upendo wa mazoezi kwa watoto wako kutoka umri mdogo. Waandikishe katika madarasa ya mafunzo ili wajifunze uwajibikaji wa pamoja na nidhamu. Mazoezi lazima liwe jambo la pili la asili kuwapa msingi wa afya kwa maisha yao yote.

20 na zaidi 

Tafuta sababu ya kusimama kila saa na kufanya mazoezi mepesi ya kujinyoosha. Tembea angalau dakika 30 kwa siku ili kufanya mwili wako uwe mwepesi. Mafunzo ya saa moja ya utimamu wa moyo angalau mara tatu kwa wiki ili kudumisha nguvu na viwango vya nguvu 

40 na zaidi

Dumisha afya ya misuli kwa mazoezi ya uimarishaji mwili mara tatu kwa wiki. Fanya mazoezi ya kutembea au kuendesha baiskeli kuufanya mwili wako kuwa mwepesi na mchangamfu.

60 na zaidi 

Kufanya mazoezi ya kawaida kama vile kutembea, kuogelea au yoga kila siku, kutaimarisha viungo vyako na kuchangia kuwa na afya nzuri ya akili na mwili. Jiunge na madarasa ya makundi ya watu wazima ili kuchangamana na kuwa mchangamfu.

BU: 

Mkufunzi binafsi Ahmed Msoma, 37, anatuwezesha kusonga mbele.

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Fumba Mbili-Wazo Moja

Find out all about new exciting seaside developments just outside Zanzibar city It’s all happening on the Fumba peninsula: Two major real estate developments creating modern living space with holiday flats and permanent family homes near the overcrowded capital. By ANDREA TAPPER Both aspiring seaside communities, started in 2015/16, fascinate locals as well as a […]
Soma zaidi
Mei 2, 2024
3 dakika.

HOW TO RUN A SUCCESSFUL AIRBNB

In Fumba Town and elsewhere in Zanzibar In 2012, Airbnb listed three apartments in Zanzibar. Today, more than 1,000 holiday apartments and villas are found on the isles: from a shipping container in Paje to a tree house in Bwejuu. Two popular Airbnb hosts in Fumba explain what works best – for them and their […]
Soma zaidi
Aprili 22, 2024
0 mins.

STREET NAME COMPETITION

Soma zaidi
Aprili 15, 2024
3 dakika.

"ZANZIBAR IS SO SUBLIME"

The son of Femi Kuti and grandson of Fela Kuti headlined one of the best Busara festivals ever By Andrea Tapper  He flew into Zanzibar, capturing the hearts of music fans from all over. Afrobeat musician Mádé Kuti, 28, and his wife Inedoye, 25, made time for an exclusive interview with THE FUMBA TIMES before […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

25 essential questions and answers to buy property in Zanzibar

READ MORE
Whatsapp Nasi