Nchi nyingi duniani zinatoa vivutio kwa wawekezaji kama vile visa ya ukazi kwa wakazi wa muda mrefu. Tanzania itachukua hatua hiyo hivi karibuni?
Suala ni wazi: Wakati wageni wanaponunua nyumba mahali fulani, iwe kwa ajili ya mapumziko, kama nyumbani mbali na nyumbani au kupangisha , wanahitaji kuhakikishiwa kuwa nyumbani kwao kwa pili ni salama na hakubanwi (huru) na masharti yoyote yale. “Itakuwa muhimu sana kwetu kupewa visa ya ukazi mara tutakapokamilisha mikataba yetu ya nyumba Zanzbar.”, anasema Milena Yanus na mpenzi wake wa kiume Graham, kutoka Ontario, Canada ambao ni wapenda michezo ya kuteleza katika mawimbi ya bahari , ambao wanafikiria kununua nyumba ya mapumziko eneo la Paje “Kazi zetu katika sekta ya kompyuta zinatuwezesha kufanya kazi popote tulipo kwa njia ya mtandao. Marafiki zangu walinunua Hispania na kurudi na kutuma fedha kila wakati, kutokana na nchi hiyo kuwapa vibali vya ukazi kirahisi kama wawekezaji.”
Katika ulimwengu wa kimtandao, nchi nyingi zaidi zinatoa visa kubwa katika kuwezesha uwekezaji. Hapo nyuma hatua ya kutoa visa na hata uraia ilionekana vigumu kwa wawekezaji wenye mtaji mkubwa, kwa sasa imekuwa kawaida zaidi, na katika upande mwingine ni mkakati mkubwa wa masoko. Katika nchi zipatazo 16 kuwa na nyumba ya makazi inakuwezesha kupata pasipoti, mathalani nchini Malta. Nchi 20 kati ya 28 za Umoja wa Ulaya, EU, zinatoa uwezekano wa makazi, unaokuwezesha kupata pasipoti baada ya muda fulani wa ukazi katika nchi husika. Panama ilikuwa na wazo kubwa la kuruhusu ukazi kwa uwekezaji wa dola $80,000 kwenye sekta ya misitu! Nchi zote hizi zinaamini kuwa kwa kuwa na sera wazi kutachochea uwkezaji wao.
“Ulimwengu unazidi kuunganika na hususan Zanzibar,kama kituo cha uwekezaji kinachotegemea utalii kwa kiasi kikubwa, kinatakiwa kurahisisha ukazi wa wawekezaji wa kigeni hapa”, anasema Hamad Hamad, 42, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara Zanzibar(ZNCC) katika mahojiano maalum na THE FUMBA TIMES (angalia kisanduku katika ukurasa huu).
Wakati utendaji wa kawaida ni kuwafanya watu kuwa taifa moja, huenda isiwe kivutio kwa nchi za Afrika, kwa mshangao inafanya kazi hata katika nchi za Caribbean na visiwa vya Pasifiki Kusini. Dominica na Vanuatu zinafurahia kuuza pasipoti kwa dola $100,000.
Makazi rafiki ya kuhamia
Sheria na kiwango cha fedha kinachohitajika kuwekeza kinakaribishwa na kinatofautiana kutoka mgeni mmoja na mwingine kulingana na aina ya ukazi wake, na ni wazi kinaonyesha namna nchi inavyovutia wawekezaji. Baadhi ya nchi zinataka wageni kuishi katika nchi zao kwa kipindi fulani maalum au kuitembelea nchi hiyo mara kwa mara:
Wakati mwingine hamu ya ukaaji au utambulisho mpya huchochewa na hali za kisiasa. Kabla ya Brexit, karibu Waingereza 128,000 walipata uraia wa Ujerumani mnamo 2019, kama vile miaka mitano iliyopita. Katika Afrika Magharibi, Ghana, ambayo ni ndoto ya kuwarejesha Waamerika Weusi kwa miongo kadhaa, serikali iliondoa ada za usajili kwa wanachama wa nje ya Afrika. Wakati wa urais wa Trump, Marekani ilituma maombi ya kuingia Ghana - nyumba ya watu milioni 29, kente cloth and legendary state founder Kwame Nkrumah – shot up from 1000 per week to a “staggering 10,000“, said Akwasi Agyeman of the Ghana Tourism Authority in a media report.
Tanzania huenda ikawa na mwelekeo sawa, kwa kuwa na waendesha mitandao ya kijamii Waafrika waishio diaspora wengi zaidi wakiitangaza Tanzania nchi ya Mlima Kilimanjaro na visiwa vya marashi vya Zanzibar na utawala wa Waafrika wengi. Katika Fumba Town, Wamarekani kadha tayari wamewekeza. Ili kuita sehemu ni nyumbani, wanachotaka ni visa ya muda mrefu.
Maelezo zaidi:
citizenshipshop.com
immigrantinvest.com
nomadcapitalist.com
escapeartist.com
“Zanzibar inatakiwa kutoa visa ya muda mrefu moja kwa moja”
Unasemaje kuhusu vibali vya ukazi kwa wageni wanaonunua mali isiyohamishika hapa?
Naunga mkono kikamilifu. Tayari suala hili limejadiliwa katika bunge la Tanzania na Zanzibar, ni suala la muungano.
Na ndipo tatizo linapoanzia…
Siyo lazima. Wakati kwa kweli ni suala la muunano, vigezo tofauti vinaweza kutumika kwa Zanzibar ambako tuna muundo tofauti wa uchumi na Tanzania bara. Tunagemea zaidi utalii.
Kiwango cha chini cha uwekezaji katika mali isiyo hamishika kinahitajika?
Ndiyo. Bei isiwe ya chini mno; mwekezaji lazima akae hapa kwa muda fulani, awekeze zaidi na kwa ujumla atengeneze mapato kwa nchi.
Kuanzia uwekezaji wa kiasi gani?
Kiwango cha chini $50,000 kinaweza kuwa sawa. Visa iwe ya kudumu. Nafikiri inaweza kupitishwa moja kwa moja!
Kuitangaza Zanzibar?
Hakika! Daima tumekuwa nchi ya ulimwengu wote. We encourage more cultural interaction with foreigners, but we will also strongly protect Zanzibar culture – after all that’s our unique selling point.