Ushirika wa wanawake wa kikundi cha Moto umedumu kwa miaka 20. Mifuko yao mipya ni moto kama ulivyo moto wenyewe.
Mifuko ya Raffia yenye mapindo yako kimitindo duniani kote. Ushirika huko Pete umebuni baadhi ya mitindo maarufu kutokana na makuti ya mnazi kwa sasa imeanza kuuzwa Zanzibar.
Miaka 20 iliyopita, mfanyakazi wa maendeleo wa Ujerumani, Antje Förstle, aliwahamasisha wasuka mikeka wenyeji kuanza kuzalisha mikeka na mifuko si tu kwa ajili ya kujipatia riziki ya kila siku bali kwa kuwauzia watalii. "Aliwafundisha wanakijiji misingi ya mikakati ya masoko na taratibu walianza uzalishaji wa bidhaa walizotengeneza kwa mikono yao, misingi ya mikakati ya masoko," anasema Dida, meneja wa ushirika wa Moto, mtu ambaye ni mwenye huruma na anayejiamini, akiwa na umri wa miaka 24 na kwa sasa anasomea shahada ya kwanza ya biashara katika chuo kikuu cha Zanzibar.
Vikapu, mikoba na mazulia yanatengenezwa kutokana na makuti ya minazi, ambayo yanavunwa, kukaushwa, kutiwa rangi(kwa kutumia rangi za asili tu) na kufumwa pembeni. Kulingana na ukubwa, inachukua wiki moja hadi kukamilika kwa bidhaa moja ya ufumaji yenye ubora wa hali juu, imetengenezwa kwa mifumo ya kijadi, imekamilika. “Kwa kweli ni ustadi halisi”, anasema Dida.
Ushirika huu pia unafuma mablanketi. Pamba inanunuliwa kutoka Tanzania bara na kutengenezwa mablanketi laini ajabu yakiwa na rangi za kupendeza. Kwa miaka mingi biashara imekua na watu wengi zaidi katika vijiji vingi zaidi wanahusishwa na biashara hii. Kwa sasa, anasema Dida, wafanyakazi wapatao 200 wengi lakini siyo wanawake tu, wanaume wanadumu na kauli mbiu ya `moto Zanzibar` katika vijiji kumi kuzunguka Pete karibu na msitu wa Jozani, ambako kazi ya uzalishaji bidhaa hizi upo. Antje Förstle pia aliwafundisha kutengeneza sabuni na jam.
Vyote hivi unaweza kununua katika ushirika wa `moto Zanzibar` katika Stone Town, mtaa wa Hurumzi. Asilimia 50 ya mapato yanawekezwa, na asilimia 50 zinakwenda moja kwa moja kwa wanavijiji. Yeyote anayenunua hapa si tu anapata bidhaa za kudumu lakini pia ni bidhaa endelevu na zenye kuzingatia ikolojia. `Moto' (Kiswahili for fire) inasimama kwenye ukweli kwamba minazi kuzunguka Pete, ambayo hutumika kwa uzalishaji wa bidhaa hizi, huenda ikaathirika kwa kukatwa na kuchomwa iwapo watu wa hapa hawatapata njia mbadala ya kujipatia kipato kutokana na kazi zao za mikono' fanyakazi kwa mtazamo halisi.
Maeneo ya uzalishaji ndani na kuzunguka Pete yanaweza kutembelewa katika ziara maalum na kuna jengo dogo la makumbusho ya kazi za uchongaji ni jambo la faida!!
Angelika Dubiel
Moto
416 mtaa wa Hurumzi, Stone Town
Wasiliana kupata duka mtaa wa Hurumzi: +255 779 388 254
Wasiliana karakana Pete: +255 773 031 178online shop: https://motozanzibar.wordpress.com/