Jumba la zamani la Sultan chini ya utawala wa mwanamke.
“Nyumba ya Pwani”katika matembezi bahari ya Shangani ni maarufu kwa mambo mengi, lakini ni watu wachache wanafahamu historia na waliosababisha kuwepo kwa historia hiyo.
Jumba la zamani la sultan lililobadilishwa kuwa mgahawa na baa, linaendeshwa na Park Hyatt, chini ya uongozi wa mwanamke. Afshan Jivraj, 34, raia wa Kenya, ambaye mababu zake wana asili ya India na Iran, alikuja Zanzibar miaka mitatu iliyopita kuangalia ufunguzi. Utafiti wake uligundua kuwa jengo hilo la ghorofa mbili lilijengwa wakati wa utawala wa sultan wa mwisho Zanzibar ambaye aliondolewa madarakani kwa nguvu mwaka 1964. ”Inasemekana aliwahifadhi vimada wake katika jengo hili”, anasema Afshan. Jengo hilo la ghorofa mbili lililo mbele ya ufukwe wa bahari, halafu likatumiwa na Waingereza kama nyumba ya uuguzi, baadaye familia za wahamiaji wa Kigoa hadi walipopata nyumba huko mpaka wakati jengo hilo lilipotelekezwa-kama ilivyo kwa majengo mengi katika Mji Mkongwe yameachwa yaoze.
“Nililipenda nilipokuwa nimeliona, anasema Afshan. Akiwa amesoma katika shule ya wasomi ya Kiswiss, akiwa na uzoefu wa kazi huko China na Dubai, alianzisha soko lakini kuanzia ngazi ya chini kabisa– kazi ambayo kila mtu asingefikiria kwa mrembo kama huyu ambaye nadra mtu asiweze kumdhania kuwa ni mpokea wageni, angefanya kazi hiyo. “Hakuna wanawake wengi mameneja wakuu katika sekta ya kutoa huduma barani Afrika”, anasema: “Kwa kweli ilibidi nipambane.” Akiwasimamia wafanyakazi 31, ambao anapenda wajihisi kama familia moja”. Pia anaratibu programu za kuwasaidia wanawake wa maeneo hayo katika Hyattxxx. “Hatukubadili muundo wowote wa jengo”, anasisiza meneja huyu. “Menyu ya mgahawa wetu ni heshima kwa historia ya utamaduni wa chakula wa Oman, India na Uingereza.”