Septemba 16, 2021
Dakika 4. Soma

Klabu ya Rotary ya Zanzibar

“Ndogo lakini hai” 

(Small but highly active”)

Miradi ya thamani ya thamani ya dola $100,000 inaandaliwa (Projects worth $100,000 in the pipeline) 

Na mwandishi wetu

Kuwasaidia wajawazito kufahamu afya ya mimba. Kuzuia saratani ya matiti. Kuwafundisha watoto Karate. Bodi mpya ya Rotary Klabu ya Zanzibar yenye wajumbe wote wanawake inaelezea miradi mipya ya klabu hiyo, dira na uimara wake.

Ikiwa na wanachama hai 18 lakini ikiwa na mamia ya wahisani inakusanya kila mwaka zaidi ya dola $30,000 katika matukio ya kuchangisha, Klabu ya Rotary ya Zanzibar inachukuliwa kama ndogo lakini ina mwamko wa juu”, kama anavyosema mwenyekiti wake anayeondoka madarakani Michael Nelson. Na zaidi inatambuliwa kuwa klabu yenye shughuli mbalimbali kuliko klabu nyingine za Rotary Afrika Mashariki, inapitisha bajeti jumla ya mwaka ya dola $100,000 kwa miradi na watu binafsi wenye mahitaji. 

Lakini nini hasa kinasaidiwa na ni namna gani ulivyo mtazamo wa kisasa wa Klabu ya Rotary kwa sasa? Ni wakati wa kuketi chini na bodi mpya ya Rotary Klabu ya wanawake wote. 

Rais mpya wa klabu hiyo ya Rotary Bernadette Kirsch anajulikana sana kwa wasomaji wa jarida la THE FUMBA TIMES kwa shughuli zake za kilimo hai katika Fumba. Katibu Shireen Jivi ni mmiliki wa kampuni ya teknolojia ya habari ijulikanayo kama “Simply IT”; mweka hazina mpya Daniela Brenco mzaliwa wa Italia, mwenye taaluma ya masoko ambaye alichukua umiliki wa hoteli ya Palace, Palace Hotel katika eneo la Stone Town. 

Hivi karibuni, mipango mitatu mipya ya klabu ya Rotary imezinduliwa kwa ajili ya wanawake na watoto. Lakini shughuli ndogo ndogo zinaangaliwa pia. Furaha kubwa kwa wanafunzi wenye ulemavu, mathalani ni uwepo wa masomo ya mara kwa mara ya muziki yanayofundishwa na walimu kutoka Shule ya Taaluma ya Muziki ya Nchi za Majahazi (DCMA). 

Ni shule yenye sifa halisi ya Rotary, kwamba klabu kutoka duniani kote zinasaidiana. Klabu ya Rotary ya Zanzibar ina bahati ya kupokea msaada kutoka klabu nyingine”, anasema Rais Bernadette Kirsch. 

Utoaji fedha- ni tatizo?

Kinyume na na kile watu wengi wanaweza kufikiria, utoaji wa fedha siyo changamoto kubwa kuliko zote, lakini ni “upatikanaji wa miradi sahihi inayotakiwa na wadhamini”, anafahamu mweka hazina Daniela Brenco. Kwa kuanzia, “ukaribu na jumuia ni mambo muhimu kuytambua ambako msaada unahitaji kweli kweli, anasema. Klabu ya Rotary ya Zanzibar ina mchakato mkali wa upimaji uliowekwa wa kuchambua miradi inayotarajiwa,” anaeleza rais Kirsch. Rotary ilianza kama maono ya mtu mmoja – Paul Harris. Mwanasheria huyo alianzisha Rotary Club ya Chicago mwaka 1905 kusaidia watu walio na mahitaji kupitia weledi wa kitaaluma. Dhamira hiyo imefanikisha kuwa na wanachama milioni 1,2 katika klabu 35,000. Jina hilo lilikuja kwa sababu mwanzoni mikutano ya klabu ilihama hama. Klabu ya Rotary ya Zanzibar ilianzishwa mwaka 2005 – miradi mipya mitatu itatekelezwa mwaka huu. 

Wajamama: Healthy mamas, 

Watoto wenye furaha-happy babies

Mbweni, eneo pendwa kwa wafanyakazi wa kimataifa na kitongoji cha mji wa Zanzibar, ni mahali pa vitu vingi lakini pia kituo kisicho cha kawaida cha jumuia ya wanawake. Kilianzishwa na kuendeshwa na Nafisa Jiddawi, maarufu wa kutoa huduma za msingi, kituo cha Wajamama kinasaidiwa na Rotary katika programu za wanawake wajawazito walio katika maisha magumu na watoto. Wanawake wanapata elimu na huduma binafsi wakati wote wa ujauzito wao. Zaidi ya wanawake 700wanatarajiwa kunufaika na huduma za ujauzito za ubora wa juu kwa mwaka. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, vifo vingi vinavyotokana na matatizo ya ujauzito kisiwa Zanzibar vinatokea wakati au mara baada ya mtoto kuzaliwa. “Huduma za wakati wa ujauzito pamoja na programu za utimamu na kuhudhuria kliniki ni mambo muhimu katika uzazi salama.”, anasema Jiddawi. “Tunahamasisha afya ya ujauzito wa wanawake na kwa undani maisha yenye afya kwa wanawake na watoto katika mpango wa rasilimali za chini.” Wajamama inawakilisha Watoto, Jamii na Mama. Mwanzilishi Nafisa Jiddawi, mwenyewe akiwa ni mama wa watoto watatu, amepitia katika kuratibu kampeni kubwa na ya haraka kukabiliana na janga la Covid, kwa kutoa elimu na vituo vya kunawa kote Zanzibar mwaka 2020

Kwa nini mafunzo ya karate kwa watoto (Why Karate is good for kids)

Sanaa ya kijeshi kama vile Karate, Aikido na Judo ni namna nzuri ya kuwa imara na afya, lakini pia kuwafunza watoto stadi muhimu za maisha kama vile nidhamu binafsi na uvumilivu katika mazingira ya kawaida na yenye afya. Klabu ya Sanaa za kijeshi ya Zanzibar ni chama kipya kilichoazaliwa, kilianzishwa mwaka 2020. Mradi huu wa jamii “Budo wenye sababu (Mradi wa BORA-BORA Project)” ulianzishwa na mwalimu wa mafunzo ya saana za kijeshi Vadim Dormidontov ambaye anasema: “Sanna za kijeshi zinafurahisha ndani yake.” Rotary wanasaidia program za Sanaa hizi katika shule tatu hapa.

Msaada wa kuzuia saratani ya matiti (Helping to prevent breast cancer) 

Asilimia 95 ya saratani ya matiti inatibika ikigunduliwa mapema. “Katika Zanzibar wanawake wanachelewa kugundua saratani hiyo, kwa hiyoidadi ya vifo inakuwa kubwa”, anasema Dr. Jenny Bouraima. Chini ya uongozi wake prtogramu ya kwanza ya ufahamu juu ya ugonjwa wa saratani ya matiti na matibabu yake ya mapema” kwa sasa inazinduliwa kwa msaada wa klabu ya Rotary ya Zanzibar. Inahusisha mafunzo ya kujipima mwenyewe kuanzisha mashauriano yanayoendelea juu ya saratani ya matiti na kuwafundisha wataalamu wa mionzi na waganga wa maeneo ya hapa hapa Zanzibar. Ruzuku inayosubiriwa ya dola $90,000 pia itahusisha vifaa vya kitaalamu kwa ajili ya upimaji wa tishu za mwili kubaini magonjwa. “Tunataka kuondoa hali ya kujirudiarudia kwa hali ya kuchelewa kugundua ugonjwa huu na vifo”, anaeleza Dr. Bouraima, mkuu wa Kliniki ya Urban Care katika Fumba Town. Uchunguzi wa awali utahusisha wanawake 600 ili kupata data Zaidi kuhusu saratani ya matiti Zanzibar. 

Rotary –ni mtindo wa zamani Zaidi kwa kizazi cha internet? 

Rotary too old fashioned for the internet age?

Kushiriki moja kwa moja na kwa mtu binafsi ni jambo la faraja”, anasema mjumbe wa bodi Daniela Brenco. “Tunashiriki kikamilifu katika jumuiya zetu”, anasema, “hatujawa wataalam katika mnara wa pembe ya ndovu.” Wanachama kama Eleanor Griplas, mmoja wa waanzilishi wa klabu ya Rotary ya Zanzibar na mmiliki wa Safari Blue, ameweka mifano kwa miaka mingi na ushiriki mkubwa katika jamii za Zanzibar. Akielezea ushiriki wa Rotary katika Zanzibar, Bernadette Kirsch anatumia mfano rahisi wa ulinganisho: “Tupo kama shangazi anayesaidia familia maskini yenye watoto, lakini hatuwi mbadala wa wazazi.” Mtaalamu wa kilimo hai anajiandaa kuleta ushirikishwaji Zaidi endelevu hapa rotary. 

Kwa mtoto kama Biko msaafa wa Rotary tayari umeonyesha athari za kudumu: Mtoto huyu wa kiume mwenye umri wa miaka 10 ana ugonjwa wa uti wa mgongo na anatumia kiti cha cha watu wenye ulemavu cha magurudumu matatu, hakuna shule yoyote ya serikali hapa Zanzibar iliyoweza kuangalia mahitaji yake ya ziada. Klabu ya Rotary imemlipia karo yake ya shule katika shule ya kimataifa ya Kiwengwa (KINS) kwa miaka mingi na walimu wamefurahi sana kusikia taarifa hiyo: “Biko ni mwanafunzi mwenye akili sana mwenye ucheshi na mwenye kupenda kujifunza.”

Shiriki hii

Makala zinazohusiana-Related Articles

Machi 31, 2021
3 dakika.

Two Fumbas – One Idea

Find out all about new exciting seaside developments just outside Zanzibar city It’s all happening on the Fumba peninsula: Two major real estate developments creating modern living space with holiday flats and permanent family homes near the overcrowded capital. By ANDREA TAPPER Both aspiring seaside communities, started in 2015/16, fascinate locals as well as a […]
Soma zaidi
Oktoba 23, 2023
2 dakika.

The unknown side of Zanzibar

Location Most secluded in Zanzibar, The Bottom Line Feel like a VIP by the ocean The road maybe rocky, but the destination rewards us for travelling it. Like a Fata Morgana, white modern villas suddenly become visible high above the sea, a wooden deck with neatly arranged cabana-like double sun beds leads to an endless […]
Soma zaidi
Oktoba 17, 2023
2 dakika.

FAKE Picture – OR NOT?

By Elias Kamau A tree house in Stone Town? Too good to be true! When we received this photo at THE FUMBA TIMES, we became highly sceptical. Here’s a guide to help you recognise fake shots – especially in your social media.  The commonsense warning is clear: don’t believe everything your Facebook and Instagram friends […]
Soma zaidi
Oktoba 3, 2023
2 dakika.

LET THE SUNSHINE IN

A German couple, one of the first buyers of a beach front house in Fumba Town, wants to start a solar business here. Engineer Ronny Paul, 44, produces custom made solar systems.  There seems to be good news on the solar front: a first photovoltaic project is planned for Bambi in the heart of the […]
Soma zaidi

Je, unatafuta mali Zanzibar?

25 essential questions and answers to buy property in Zanzibar

READ MORE
Whatsapp Nasi